MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
Umenikuna kwa hoja yako.Kama Watanzania wote mnaosoma hoja za JF mna nia njema na nchi hii msishabikie kabisa EL kuanzisha TV kwa si kwa nia njema kwa anachowaza yeye ni uongozi tuu wa nchi hii wakati ni fisadi na ni mtu wa visasi.Naomba sana CHADEMA,MENGI na Waandishi makini tushirikiane tuhakikishe mafisadi hawatambi katika nchi hii.EL na mafisadi wenzake ni kama MOBUTU,ABACHA na wahujumu wengine wa uchumi wa nchi zao.Mungu ibariki TZ.Kwa kweli kama ni kwa nia njema, hakuna ubaya kwa Lowassa kuanzisha TV popote iwe Dar ama Arusha. Lakini jambo moja ambalo lazima tuliangalia kwa makini ni kwamba hawa jamaa wamepania kuchukua nchi. Mind you "kuchukua nchi" na hawatanii, mnataka ama hamtaki. Kilichompata Lowassa na wenzake, wameona ni kutokana na nguvu ya media. Wameamua sasa na mumesikia ama kuona, magazeti kibao yakiongozwa na ununuzi wa New Habari. Wamenunua Channel Ten. Hatua itakayofuata na ambayo mchakato umeanza ni kuwadhibiti wamiliki wa vyombo wanavyoona itakuwa kikwazo kwao ikiwamo IPP Media.
Kwa ufupi ni kwamba kama tukiwa makini kidogo tu tutabaini kwamba, Tanzania yetu inaelekea kubaya. Tunajua kila mtu ana haki ya kutawala, lakini si urithi Mwalimu Nyerere aliotuachia kwamba uongozi ni kwa wenye fedha na vizazi vyao. Nawaambia hata ndugu zangu humu (Nawafahamu) ambao wana nia njema ya kuja kuingia katika siasa kihalali (wakiwamo wanaoshabikia EL kuanzisha TV) wajue kwamba bila fedha (za rushwa) hawatashinda kutokana na mfumo uliojikita na unaoendelea kuimarika vinginevyo wawe vibaraka wa wenye fedha. Hii ni HATARI sana na hapa tukijadili mambo tuangalie huko (2010-2020) maana wenzetu wamejipanga hivyo na kwa gharama zozote zile ikibidi hata za HATARI (nitajadili kwa wakati).
Hiyo Serikali ilikuwa inaongozwa na nani kama si EL.Anzia tangu enzi za AICC na kitengo cha maafa Ofisi ya PM Lowassa alizuia wapi ufisadi,sasa hiyo TV kama si kulindia fedha alizokwapua.Ni vema asome alama za nyakati,hawezi kuongoza nchi hii labda atafute kibaraka kama alivyofanya kwa JK na kumkandia Dr.Salim.kuupinga ufisadi si kupinga kila kitu kinachofanyika au kufanywa na hawa watu...kufungua redio jamani ni katika investment RAHISI sana hapa nchini kufanya, kama kuna mtu hajui aulize pale TCRA.
mi naona ni kitu cha kumpongeza na kumtaka aitumie kwa maendeleo ya eneo lile..tusiwe sana negative tukazani ndio mtazamo sahihi na kupinga hata vitu visivyo na nia mbaya kwa kutumia jazba la ufisadi....
ufisadi ulitengenezwa na serikali tuliyoiweka sisi wenyewe kwa kushindwa kusimamia rasirimali za nchi....tukumbuke kukumbatia maji kama jiwe ni ujinga...
CCM ni taleban wa ufisadi!-Kobani haki yake kuwekeza anavyotaka na hakuna ubaya wowote ili mradi atafuata sheria zote za Media na kodi,mengine humu naona ni majungu tuu,kama mna kesi mbona mlishindwa kumweka ndani alivyojiuzuru!
acheni kelele.. sinamnalalamikaga mafisadi wanainvest out of the country only.. sasa lowassa anaemploy watu wangapi kwenye majumba yake 50, viwanda, makampuni ya alphatel, alpha high skul, alpha dry clearners, ranch yake, voda, sijui nini.. and all the rest that few know about...! Mtu akiwa mwizi sio maana yake kila alichonacho kaiba.. The man actually has what can be decribed as a business empire and regarless of how he got it (and I'm not defending him here.. kwakuwa simpendi na sikubaliani na vitu alivyo-anavyo fanya).. the fact remains anawalisha watanzania wengi.. more than all the people wasioiba maana who is to say wangeziona hizo hela anyway.. Political camps blind people from the cold facts sometimes.. (Lowassa is a cancer lakini kuweni objective mnapoongelea haya mambo ama hii JF nayo itakuwa genge tuu la wapayukaji if its not that already... and I seem to be convinced of the latter, the majority of the time nowardays..)
Yessir,
subiri ina kuja orodha ya member wa JF wanao tumiwa ha baadhi ya watu hapa,
Umenikuna kwa hoja yako.Kama Watanzania wote mnaosoma hoja za JF mna nia njema na nchi hii msishabikie kabisa EL kuanzisha TV kwa si kwa nia njema kwa anachowaza yeye ni uongozi tuu wa nchi hii wakati ni fisadi na ni mtu wa visasi.Naomba sana CHADEMA,MENGI na Waandishi makini tushirikiane tuhakikishe mafisadi hawatambi katika nchi hii.EL na mafisadi wenzake ni kama MOBUTU,ABACHA na wahujumu wengine wa uchumi wa nchi zao.Mungu ibariki TZ.
Hivi hii orodha ilishatolewa?
Hiyo orodha mbona ilitolewa mda sana ndugu, pole sana kama hukuipata.
Wewe Bwana, anunue tu ziwepo nyingi hizo. Tupo wengi hivi sasa- unafikiri sote tunaweza kujibanza ITV na kwa Tido tu. Wacha wigo upanuke - tunahiataji ajira Bwana.Alishanunua RAdio 5 ya Arusha. Mikakati ndio hiyo.Sii ajabu akaibukia mgombea binafsi.