Lowassa (mb) asema uongo hadharani (apotosha live)

Lowassa (mb) asema uongo hadharani (apotosha live)

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
1,459
Reaction score
699
Edward Lowassa, amesema matumizi ya fedha zilizorudishwa nchini, baada ya ununuzi wa rada, maarufu chenji ya rada, hayaeleweki vizuri.

Alisema hayo juzi katika mkutano uliojumuisha wadau wa elimu, unaofanyika kila mwaka wilayani Monduli mkoani Arusha ili kuangalia changamoto na mafanikio ya elimu wilayani humo. Lowassa alisema moja ya mambo yanayomsikitisha ni kuona fedha hizo, zikielekezwa kwenye ukarabati wa majengo, badala ya kujenga majengo mapya. Mara nyingi ukarabati unatumia fedha nyingi, bila kuwa na maelezo mazuri, tofauti na ujenzi wa majengo mapya. Ningefurahi kuona fedha za rada zikitumika kujenga jengo la maktaba, maabara au basi nyumba za walimu. Lakini ukisema unazipeleka kwenye ukarabati, fedha zitapotea,alisema Lowassa.

Tunamshangaa Lowassa kama mbunge na walishaelezwa bungeni kuwa fedha hizo zimeelekezwa kununua vitabu ambavyo mchakato wake unaendelea na kununua madawati ambayo tamisemi wametangaza zabuni wiki iliyopita magazetini
. Sasa kwa nini awapotoshe wadau hawa wa elimu? Haoni anachonganisha serikali na wapiga kura? Je ni jengo lipi limekarabatiwa kwa fedha ya chenji ya rada? Toa takwimu sahihi mheshimiwa.
 
Kujadili jinsi chenji ya rada inavyotumika ni sawa, lakini mbona maswali ya msingi tumeyasahau: Kumbekeni kuwa Mh. Chenge anayo sehemu ya hiyo chenji, alizoziita vijisenti, na hakuna sasa hivi anayemwambia arudishe na sheria kuchukua mkondo wake kama mtumishi wa umma wakati huo. Pili, serikali ya CCM tangu waziri wa uingereza mwaka 2002 alipopiga kelele za wizi huo ilimkejeli na kukaa kimya. CCM na serikali yake ina mamlaka gani ya kimaadili (moral authority) kuzungumzia matumizi ya fedha hizi?
 
Manaibu waziri wawili walichanganya Bunge


  • Ni kuhusu chenji za rada
  • Mmoja asema zimetumika , lakini mwingine akataa.

Dodoma.


Manaibu Waziri wiwili jana walipishana katika majibu yao kuhusu fedha za rada na kujikuta wakitoa majibu tofauti hali iliyowachanganya wabunge na kusababisha baadhi kuomba mwongozo. Hali hiyo ilitokea ndani ya Bunge baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene kueleza kuwa fedha za rada hazijagawanywa kwa kuwa bado kuna taratibu ambazo zinatakiwa kufanyika. Mbene alitoa kauli hiyo kufuatia swali la nyongeza la Moses Machali aliyetaka maelezo kuhusu tetesi kuwa ziko kampuni ambazo zimepewa tenda ya kununua vitabu na madawati. "Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la mbunge kama ifuatavyo, hadi sasa fedha hiyo haijagawanywa kwani bado kuna mambo ambayo yanahitaji kukamilishwa," alisema Mbene.


Kutokana na majibu hayo, ilimlazimu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa kusimama na kulieleza Bunge kuwa fedha hizo tayari zimeshagawanywa na kuanza kufanya kazi.


Majaliwa alisema kati ya fedha hizo, Sh 55.2 bilioni zimepangwa kununua vitabu kwa Tanzania Bara, na Sh 18 bilioni zitanunua madawati tenda ambazo zimetolewa kwa kampuni tisa.

Source: Mwananchi Manaibu waziri wawili walichanganya Bunge - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz
 
Back
Top Bottom