Elections 2015 Lowassa: Serikali yangu itaangalia jinsi ya kuvunja mkataba wa bandari ya Bagamoyo

Wanaishangilia leo wanafikiri wanamkomoa Magufuli lakini Muda utaongea.

..mliwachochea kuamini hivyo.

..kila alichokifanya Magufuli mlikuwa mkichomekeza kwamba ni kwa ajili ya kuwakomoa wapinzani.
 
Kwa hiyo sasa hivi mnamkomoa magufuli?

..kwani Magufuli alikuwa anawakomoa Chadema?

..Mataga kama hamkubaliani ni mwenyekiti wenu mnayo haki ya kumpinga.

..Na mkishindwana naye mnao uhuru wa kuanzisha chama na kuendeleza harakati zenu.

..Sio sahihi au busara kuwasubiri Chadema wawasemee wakati mmekuwa mkiwabeza na kuwapinga kwa muda mrefu.
 
Nyumbu bhana! Kukosoa ni kutokubaliana na mtu?

Ndio maana hapo chadema mbowe akisema basi nyie hufuata tu bila kuhoji?
 
Nyumbu bhana! Kukosoa ni kutokubaliana na mtu?

Ndio maana hapo chadema mbowe akisema basi nyie hufuata tu bila kuhoji?

..kumkosoa mwenyekiti wa ccm ni haki yenu.

..kutokukubaliana na mwenyekiti wenu sio dhambi.

..mataga mnaowajibu ktk chama chenu msiukimbie.
 
..kumkosoa mwenyekiti wa ccm ni haki yenu.

..kutokukubaliana na mwenyekiti wenu sio dhambi.

..mataga mnaowajibu ktk chama chenu msiukimbie.
Si ndio kama hivi tunawajibika kukosoa ila nyie nyumbu mnapinga kukosoa na mnamsifia sana ili kumkomoa marehemu?
 
Si ndio kama hivi tunawajibika kukosoa ila nyie nyumbu mnapinga kukosoa na mnamsifia sana ili kumkomoa marehemu?

..mataga mlikuwa mnasifia hata ukatili wa Magufuli.

..siyo jambo la ajabu kuwepo kwa kikundi kinachomsifia Mama Samia ktk kila analofanya, hata pale anapokosea.

..Huu ni wakati wa Mataga kujipambanua kama vijana mliokomaa kifikra ktk kulitetea taifa lenu.
 
Si ndio hivi tunalitetea ila nyie nyumbu mmejipambanua kumpamba na kusema yuko vizuri sana?
 
Ule ukaskazini ndio unadhihirika rasmi..

To deny development at Pwani region!

Funny enough hajui kuwa kuna wachaga waliowekeza Bagamoyo !!

Mkiitwa Genge mnachukia...mkiambiwa hana uwezo mnakasirika!

Makuwadi na makasuku wa mamlaka vipi kwa Magufuli msimamo wako ulikua upi na Leo kwa SSH ni upi?
 
Mmoja aliuza nyumba za serikali kimagumashi na kujenga airport kijijini kwake.

Mwingine alituingiza chaka Richmond

Muacheni mama afanye kazi yake
 
Unaanzisha thread ya kusapoti dakika 5 baadaye unaanzisha ya kupinga, kazi unayo.
 

Mkuu Elitwege unakuwa hueleweki. Nikadhani ufafanuzi wako mwenyewe ingependeza zaidi kwenye uzi huu:


Kama ikikupendeza mkuu.
 
Mleta mada wewe ni kati ya waTz waloifikisha nchi hii hapa kuzimu. Mnapoishangilia Ccm kwa kuitawala nchi ipendavyo ndiyo matokeo yake haya.

Mfano kuna haja gani mikataba muhimu ya nchi kama huu kuwa SIRI kubwa ?!. Hapa ndipo penye uchochoro wa mambo ya kijinga kama haya unayolalamikia. Mkapa alionywa na wanaharakati enzi za mikataba ya madini. Hakumsikia mtu , badala yake aliwakebehi kuwa ni wavivu wa kufikiri .

Muswaada wa Gas na mafuta . Wapinzani na waTz wenye nia njema walionya na kuikataa . Kilichotokea wabunge wa Ccm kupitia spika wao Mama Makinda waliipitisha usiku wa manane Maghufuli na Lowassa wakiwa sehemu ya wabunge hao. Leo tunailalamikia mkataba huo. Tatizo ni mfumo wa uongozi wa Ccm na katiba mbovu inayommilikisha Rais nchi.
 
Kumbe hata UKAWA tungaliwapa nchi mwaka 2015, mradi huu wa bandari ya Bagamoyo wangaliufutilia mbali na hatungaliweza kuu retrieve. Yaani UKAWA wangaliu delete hadi na kwenye dustbin. Angalao CCM hawakuu delete kule kwenye dustbin na ndiyo maana tumeweza kuu restore. Hongereni CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…