hivi mfano ujue ndugu/rafiki yako ni wanted na watu fulani.
Na unajua kabisa alifanya kosa, kama ukifahamu alowakosea wanatafuta details zake, utawapa hizo info?
Kuna hii kitu loyalty(faifhfulness/commitment to obligation) kati ya marafiki iwe wenye mahusiano ya kimapenzi ama urafiki kwa maana ya urafiki tu.
Kati ya marafiki 'loyalty' ina umuhimu kiasi gani?
Na mfano mtu akashindwa kuwa loyal mara moja je kuna jinsi ya kurudisha hali ya awali?
Hii dhana/neno huwa linanichanganya sana hasa katika kuliishi na jamii ya marafiki.
Na unapogundua rafiki/ndugu yako amefanya crime utamuumbua au loyalty inatakiwa ichukue nafasi yake?
Naomba msaada wa kudadavua.
Hiyo kitu ni muhimu kwa marafiki au hata wapenzi, tatizo ni kwamba marafiki wengi huwa hawashibani kiasi cha kuweza kufichiana siri. Hakuna urafiki wa dhati, watu huwa marafiki huku akitaraji maslahi fulani au hayo maslahi ndio yanaendesha urafiki. Kama ni rafiki wa dhati hutopenda aingie kwenye matatizo na utakuwa tayari kwa lolote hata kama wewe ndio utaingia kwenye risk.
Nakupa mfano wa kweli ambao nimeona marafiki waliopendana.
Kulikuwa na wakaka wawili wote wapo chuo na walikuwa marafiki kupita kiasi. Mkaka A alikuwa mbovu wa hesabu ila mkaka B alikuwa nondo kila somo. Mkaka A ilikuwa kwa vyovyote lazima asupp math na angesupp asingechomoka lazima angecarry na pia asingechomoka ni lazima angedisco.
Katika kusaidiana wakati wa UE mkaka B akafanya mtihani kwa kuandika examination namba ya A na mkaka A akaandika ya B. Matokeo yametoka kukawa na supp, mkaka B alisupp maana alifanyiwa paper na mkaka A ambae alikuwa kilaza.. Mkaka B ikabidi asapue ile pepa ila alijikerisha ili asiwekewe C.
Swali: ni wangapi wanaweza kujitoa kwa kiasi hicho? Jibu ni wachache sana.
Haya, mmoja mmoja aniambie amejifunza nini.
mi nimejifunza, kumbe upo form2B unafikiria sapu sijui keri ndo vinini ivyo?
mi nimejifunza, kumbe upo form2B unafikiria sapu sijui keri ndo vinini ivyo?
anko unazeeka kumbukumbu. Umesahau ile thread yangu ya kufaulu form 4? Nilikuwa form 4b, sahivi naingia form 5 hayo masupu na machapati huwa namsikia senetor. Lol
Kaka nimekumisi. Msalimie wifi. Naona unataka kuchangia ada hapo
Ayaaa kumbe nimeshasahu uzee unaingia vibaya..sasa hapo naona umeshamsingizia Senator....Umemsinkia King apo juu?
king siongei nae nimemnunia. Hlf zeeka ili usitoke mvi, na uhakikishe hautupi shida wapwa.
mmh..shida kama zipi kwa mfano..
Na unapogundua rafiki/ndugu yako amefanya crime utamuumbua au loyalty inatakiwa ichukue nafasi yake?
Nilikua sijawahi fikiria hivi ila this is the explanation kabisaaaaa.Huwa wanasema "loyalty in friendship is tested when boldness is required." Kwa mfano kama ndugu/rafiki yako ameua na anatafutwa na polisi lakini wewe umemficha. Je, uko tayari kushtakiwa na kufungwa kwa kosa la accessory after the fact? Accessory after the fact is the one who aids a criminal after the commission of a crime, but was not present at the time of the crime. Kama uko bold enough kuhukumiwa na kufungwa kwa kumficha, basi utakuwa una loyalty kwake. Kama hauko tayari kumficha na ukaamua kumripoti polisi basi huna loyality kwake.
Lakini kitendo cha kumripoti inawezekana loyalty yako sehemu nyingine. Kwa mfano, kwa kawaida huwa kuna loyalty kati ya mwajiri na mwajiriwa. Lakini ukija kwenye ethics za whistleblowing unakuta kuna conflicting multiplicity of loyalties. Loyalty ya mwajiriwa inaweza kugongana na loyalty yake kwa jamii nzima kwa ujumla hasa pale practices za biashara yake zinapo-affect jamii. Kwa hiyo kitendo cha wewe kutomficha na kuambua kumripoti ndugu yako polisi ina maana kuwa loyalty yako iko zaidi kwa jamii.
Nafikiri loyalty kwa mtu fulani inakuwa ngumu pale ambapo ina-conflict na loyalty nyingine.
Nilikua sijawahi fikiria hivi ila this is the explanation kabisaaaaa.
Shkamoo Uncle. Mbona unaguna?mmmmmh
Shkamoo Uncle. Mbona unaguna?
Haujakubaliana na EMT?
Huuuushhhhh... I think he is sleeping 🙂wachakachuzi nendeni chit chat.
@EMT, nadhani umenipa mwanga mkubwa, thanks.