Lubuva anatangaza matokeo ya rais wa nchi gani ??

bucho

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2010
Posts
5,149
Reaction score
3,209
Wanasheria naomba msaada wenu kujua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anatangaza matokeo ya uchaguzi wa Tanganyika ama wa Tanzania ? Kama ni wa tanzania mbona uchaguzi wa Zanzibar ulishafutwa ??

Swali...

Je kuna uhalali wowote wa yeye kuendelea kutangaza matokeo wakati upande mmoja wa muungano umeshafuta matokeo yake ?? Ama haya matokeo anayoyatangaza ni ya uchaguzi wa Tanganyika tuu ??

Naomba msaada wenu wakuu maana uwelewa wangu ni mdogo kuhusu hili swala..
 
Ningependa kusikia kutoka kwa wataalam wanaojua sheria kuhusu hili
 
Hata pia na mimi ningependa kusikia kuhusu ile tundu lisu mbona kwenye hili kimya?
 
Tanzania imegawanyika kuna Tanzania bara NA Tanzania visiwani.Matokeo yanayotangazwa na Lubuva ni ya Tanzania bara..natumaia nimewajibu.
 
Tanzania imegawanyika kuna Tanzania bara NA Tanzania visiwani.Matokeo yanayotangazwa na Lubuva ni ya Tanzania bara..natumaia nimewajibu.

Mkuu,Rais atakayeshinda atakuwa ni wa Muungano au Tanzania bara tupu na kama ni wa Bara tupu kura za muungano walizopiga wazenji zinaenda wapi??
 
Nec si zec.urais wa muungano unasimamiwa nec hivyo kauli ya zec ni kwa uchaguzi unahusu serikali ya mapinduzi ya znz si serikali ya muungano
 
Tanzania imegawanyika kuna Tanzania bara NA Tanzania visiwani.Matokeo yanayotangazwa na Lubuva ni ya Tanzania bara..natumaia nimewajibu.

Twende utaratibu mkuu.... Kwahyo kumbe ni matokeo ya nchi ya Tanzania bara sio ya Tanzania ??? Kama ni hvyo sawa nimekuelewa. Ila katiba yetu haina nchi ya Tanzania bara
Tunayo jamuhuri ya muungano wa Tanzania tu
 
Wewe bwana weweee!.....Shamba la Bwana Heri, Minazi ya Bwana Heri, wewe Mpwapwike utafanya nini?
 
Mkuu,Rais atakayeshinda atakuwa ni wa Muungano au Tanzania bara tupu na kama ni wa Bara tupu kura za muungano walizopiga wazenji zinaenda wapi??

KWani raisi wa Tanzania visiwani,ana mamlaka gani akiwa bara?
 
Lubuver na tume yake sijui wanatoka Sengerema. Maana Kila mzanzibari alipiga kura tano, Sheha, Mwakilishi, Mbunge wa Muungano,Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kura zote alipiga siku moja, kituo kimoja na kwa kadi moja. Sasa kama matokeo ya Sheha, Mwakilishi, Mbunge wa Muungano na Rais wa Zanzibar ni batili sasa yale ya Uraisi wa muungano yanaendeleaje kuwa halali kama baadhi ya dosari alizosema Jecha zilijitokeza vituoni?
 
Mtajibeba......
Magufuli anaapishwa kesho Uhuru stadium.
 
Nec si zec.urais wa muungano unasimamiwa nec hivyo kauli ya zec ni kwa uchaguzi unahusu serikali ya mapinduzi ya znz si serikali ya muungano

swali,kama kura zilizopigwa visiwani zimefutwa atapatikana vipi raisi wa bara?
 
Nec si zec.urais wa muungano unasimamiwa nec hivyo kauli ya zec ni kwa uchaguzi unahusu serikali ya mapinduzi ya znz si serikali ya muungano

Unajichanganya mkuu??? Kama NEC haihusiani na Zec kwanini wa Zanzibar wapige kura za rais wa muungano ??? Bac Kutakuwa hakuna uhalali wa wao kupiga kura za kumchagua raise wa muungano bac.
 
Tanzania imegawanyika kuna Tanzania bara NA Tanzania visiwani.Matokeo yanayotangazwa na Lubuva ni ya Tanzania bara..natumaia nimewajibu.

Hapo maana yake mshindi atakuwa Rais wa Tanganyika, itabidi ufanyike uchaguzi mwingine wa kutafuta Rais wa Tanzania
 
Yanii hapo tu pakufuta matokeo ya zanzibar na mm sielewi kama hayo matokeo anayotangaza lubuva ni ya JMT au tanganyika wanasheria msaada wenu tafadhari
 
KWani raisi wa Tanzania visiwani,ana mamlaka gani akiwa bara?

Mkuu hatuongelei Mamlaka ya Rais wa Zanzibar akiwa bara,tunazungumzia ya kwamba Wanzanzibari walipiga kura ya Serikali ya Muungano,hakuna nchi ya Tanzania bara popote Duniani,bali kuna nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na ndiyo maana Magufuli alikuwa na mgombea mwenza mzanzibar Mama Samia Ally na Lowassa alikuwa na Haji Duni,hii yote ni kuleta taswira halisi ya Muungano,ukifuta kura zao za Muungano maana yake hakuna muungano tena na hivyo basi mnawapa uhalali wa wazanzibari kuudai uhuru wao kamili kwa kuwa hata kny uchaguzi mmewadharau,hauoni hatari hii Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…