Luc Eymael, Papi Tshishimbi wapigwa faini. Waamuzi wa mchezo wa Yanga na Polisi wafungiwa. Masau Bwire apelekwa Kamati ya Nidhamu

Luc Eymael, Papi Tshishimbi wapigwa faini. Waamuzi wa mchezo wa Yanga na Polisi wafungiwa. Masau Bwire apelekwa Kamati ya Nidhamu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Msemaji wa Timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari na kauli za maudhi kwa viongozi wa timu ya Polisi Tanzania FC katika mchezo uliochezwa Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.

Mechi namba 240- Coastal Union 0 FC vs Yanga SC 0: Kocha wa Yanga Luc Eymael ametozwa faini ya Tsh 500,000 (laki tano) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano (interview) na mdhamini wa Ligi Kuu Azam Media katika mechi iliyofanyika Februari 23, 2020 uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 41(2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Mchezaji na nahodha wa timu ya Yanga SC Papi Tshishimbi ametozwa faini ya Tsh. 200,000 (laki mbili) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano (interview) na mdhamini wa Ligi Kuu Azam Media katika mechi iliyofanyika Februari 23, 2020 uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga.

Adhabu imetolewa kwa uzingativu wa kanuni 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Mchezo namba 233 (Polisi Tanzania vs Yanga SC): Waamuzi waliosimamia mchezo namba 223 Polisi Tanzania vs Yanga SC Abel Willium na Martin Mwalyaje wamefungiwa miezi mitatu (3) kwa kosa la waamuzi hao kushindwa kutafsiri sheria mchezo huo tajwa uliofanyika Februari 18, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.

Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 39(1A) ya Udhibiti wa Waamuzi.
 
Samahani sana JF, Mbona kama kuna double standard katika hizi adhabu kwa waamuzi baada ya kufanya makosa yanayofanana (kushindwa kutafsiri sheria 17)? Mwamuzi mmoja alifungiwa miaka 3 na sasa wengine wanafungiwa miezi 3?

Ahsante
 
Haji Manara kwa nini hawamfungii kwa kuidhalilisha YANGA kila siku? hawa TFF ni wapuuzi tawi la simba
 
Haji Manara kwa nini hawamfungii kwa kuidhalilisha YANGA kila siku? hawa TFF ni wapuuzi tawi la Simba
 
Jeri muloo fc wamesusa kufanya mahojiano baada ya mechi. asa mnamnunia nani na mpira mmecheza wenyewe. Mijinga kabisa😡
 
Jeri muloo fc wamesusa kufanya mahojiano baada ya mechi. asa mnamnunia nani na mpira mmecheza wenyewe. Mijinga kabisa😡
Mr Aussens alikuwa sawa kuwaita mikia uneducated..Tshishimbi kavurugwa wakati captain msaidizi Juma Abdul yupo..kwa nini Azam media wakata aongee captain tu?
 
Wasipukuwa makini watafungia waamuzi wote, hawajui kuwa waamuzi wanakamgomo kao ka kudai malipo ndio maana wanachezesha ovyo, sasa wakiwafungia wote karia inabidi akachezeshe yeye.
 
Uamuzi mgumu pale ukizingatia wamo wenye makosa. Kama Wawa, kagere na mkude

Haya yote yanatakiwa kutolewa maamuzi ya haki bila kuangalia mchezaji ni wa timu gani na ndipo nidhamu itakaporudi uwanjani, sasa hivi yaani mtu unaangalia mpira na kufurahia vizuri tu lakini ghafla mchezaji nguli na makini eti anampiga kiwiko mwenzie au anamkanyaga kwa makusudi tena kishamba shamba tu kwanini hawa hawapewi adhabu stahili kwa wakati muafaka au TFF wanasubiri waingize pesa hiyo tarehe 8 ndio watoe adhabu?
 
Mr Aussens alikuwa sawa kuwaita mikia uneducated..Tshishimbi kavurugwa wakati captain msaidizi Juma Abdul yupo..kwa nini Azam media wakata aongee captain tu?
Mnatumia nguvu nyingi sana kutetea ujinga. Kavurugwa huyo shishimbi ndo alivyokwambia? Na hii ndio sababu iliyomfanya yeye akatae mahojiano ya dakika mbili? Jeri muloo FC
 
Back
Top Bottom