BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Awali, Lucia alikua Makamu wa Rais wa shirika hilo.
Taarifa iliyotolewa ya Januari 8, 2023 inasema kuwa uteuzi wa Lucia kuwa Katibu Mtendaji kwa miaka mitatu umeanza rasmi
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa sheria kipengele cha 37 (1) cha Kamati Kuu ya Taifa ya Shirika hilo (NEC)
Lucia, ambae ana uzoefu wa miaka 17 katika masuala ya uongozi, amewahi kufanya kazi katika Kampuni mbalimbali mbali kama Meneja Rasilimali Watu na usimamizi wa vifaa.
Baadhi ya Kampuni alizowahi kufanya kazi ni Tata Holding Ltd, Logistics, Dar es Salaam Corridor group, Kampuni ya madini ya Tanzanite One, Accasia na Barrick.