Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Huyu ni Mtawa wa Kifaransa, Lucile Randon. Ana umri wa miaka 118 na ndiye mtu mzee zaidi ulimwenguni. Alizaliwa tarehe 11.02.1904.
Marafiki zake wote, na jamaa aliowajua wameshakufa. Yeye ni kipofu na anatembelea kiti cha magurudumu.
Kwa sababu ni mtawa, hivyo hana watoto wala wajukuu. Mnamo 2021, alisema anatamani angejiunga na jamaa zake mbinguni.
Randon alipokea zawadi kutoka kwa Emmanuel Macron katika siku yake ya kuzaliwa ya miaka 118 mnamo Februari 2022. Lakini aliona kuwa "heshima ya kusikitisha" kwani "ingekuwa bora zaidi kama angekuwa ameshaenda mbinguni".
Unaweza kuwa mpweke sana katikati ya watu. Mwili wake uko katika ulimwengu huu lakini moyo wake haupo tena hapa.