SoC03 Luck and Choices

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 3, 2022
Posts
13
Reaction score
13
LUCK and CHOICES
Hakuna mtu ambaye hajawahi kusikia neno BAHATI(LUCK) ,.Ila Hakuna kitu Bahati Lakini Kila kitu ni Bahati. Wazungu wanasema Bahati ni Sawa na Fursa ukaongeza na maandalizi ya hiyoo Fursa
(Luck = Opportunity +Preparation).

Yaani ili uwe na Bahati basi ni lazima uwe na maandalizi juu ya Fursa Fulani ambayo unaitaka. Billionea Elon Musk aliwahi kusema kuwa LUCK is Labour Under Correct Knowledge akimaanisha Fanya Kazi Katika Maarifa Sahihi, Sio mtu umesomea Ualimu ila unataka Bahati ya kuajiliwa Kama Mwanasheria.

Hilo halitawezekana maishani utaishia kusema tu ohhhh mimi Sina Bahati, wakati wewe mwenyewe hujajiweka kibahati. Leo hii Ntakuelezea namna na jinsi yakuwa mtu mwenye Bahati kuliko mtu mwingine yeyote yule Dunian

1.Jiamin, Chochote unachokifanya amini kuwa utafanikiwa nacho hata kama watu watakwambia huwezi kufanikiwa katika jambo hilooo wewe Jiamini na tilia mkazo na nguvu Zaidi Lakini ili ujiamin ni lazima uwe na elimu na uhakika juu ya Jambo unalolifanya.

2. Usikate Tamaa, Binadamu huwa hatufanikiwai na kujihisi kama hatuna Bahati kutokana na kukata Tamaa mapema juu ya Jambo Fulani tunalotamani kufanikiwa kwa haraka Sana hivyo ni lazima tuwe wavumilivu.

3.Mwamini Mungu, Wazungu wanasema Pray Trust and Wait (Sali Amini na Subiri) Watu wengi huwa Tunasali Tunamini Lakini Kwenye kuwa na Subra tu Binadamu wengi hatuna Subra mwisho wa siku tunaishia kusema ahhh mimi Sina Bahati.

4. Kuwa na Mtazamo Chanya katika kila kitu Ukiwa na Mtazamo hasi katika Fursa Fulani kamwe hautaweza kuwa na Bahati katika maisha yako

5.Tabia Nzuri Ni lazima uwe na nidhamu kuheshimu watu na kujiheahimu wewe mwenyewe pia katika kila kitu unachofanya ndipo utakapokuwa mtu mwenye Bahati.

Ukijiona au kujihisi kama wewe hauna Bahati basi ujue hayo mambo matano hapo juu huyazingatii hata kidogo,Sasa ili uwe wa Bahati ni lazima uyazingatie hayo mambo Hakuna mtu mwenye Bahati na wala asiyekuwa na Bahati wote tukiyafanya hayo mambo tutakuwa na Bahati.

Kuna watu wanadiliki kuamini kuwa ili uwe mtu wa Bahati ni lazima uende kwa Mganga wa kienyeji ili aweze kusafisha nyota yako na uweze kuwa mtu mwenye Bahati, Labda nikuibie siri Ndugu yangu hapo unadanganywa tu na huyo Mganga atakula hela yako Bure ni bora hiyoo Fedha hata ukanunua Nyama ili uweze kula na watoto wako tu maana kama hautaweza kuwa na maandalizi yakutosha juu ya Fursa Fulani usahau kabisa kuwa mtu mwenye Bahati na Mganga ataendelea kula Fedha zako tu. Hivyo Hakuna kitu Bahati ila kila kitu ni Bahati kwa kutokana na maandalizi yako juu ya Fursa

CHOICES
Chaguzi (Choices) kila kitu tunachokifanya katika maisha yetu kimetokana na Chaguzi, Hakuna mtu ambaye anafanya jambo Fulani bila yakuwa na Chaguzi na Baada ya Chaguzi tunakitu kinaitwa Chaguo. Chaguo ni nini Chaguo ni maamuzi yanayoamuliwa kutoka pande mbili au zaidi ya mbili. Nchi zote Duniani huwa tunafanya uchaguzi wa viongozi wetu na Baada ya uchaguzi huwa tuna mshindi mmoja ambaye ametokana na Chaguzi Zetu ambaye pia tunaweza kumwita Chaguo Letu.

Ndio maaana kama Kiongozi fulani aliyechaguliwa akifanya vibaya watu huwa wanajilaumu kwa uchaguzi mbaya walioufanya na hata Kiongozi akifanya vyema wananchi watajisifu kwa kuchagua vizuri,Hivyo basi katika maisha yetu haya ya kila siku tunakumbushwa kuwa makini Sana na vitu ambavyo tunavichagua katika kila kitu/Fursa maana ukichagua vibaya basi mabaya yatakukuta na ukichagua mema, mema pia yatakukuta.

Lakin Kuna watu hawajui ni nini wafanye ili waweze kuwa na Chaguzi nzuri katika maisha Yao Leo ntakujuza na kukufunza namna ya kuwa mchaguaji mzuri ili badae usije Sema sikukuambia.

1.Kuwa Mpole na Makini Sana, Usije ukajaribu kupanick Katika kufanya maamuzi yako Tena ufanye maamuz au Chaguzi akili yako ikiwa haina mawazo wala stress za Aina yoyote ile na pia usichague kwa kulazimishwa na mtu au watu just kuwa Mpole na utulie Sana.Na jipe muda wa kufikilia vizuri juu ya jambo unalotaka kulichagua tambua faida na hasara zake mapema kabla ya kuchagua.

2. Shirikisha watu, kama utafika hatua utaona uwezo wa akili yako umefikia mwisho na bado haupati jawabu sahihi basi jaribu kuweza kuwashirikisha watu ambao unajua wanautaalamu au ufahamu juu ya jambo unalotaka kulichagua kwa maana Hakuna jambo ambalo litakuwa jipya kufanyia Duniani hivyo Shirikisha watu wenye uzoefu zaidi.

3.Orodhesha Chaguzi zako, ukiweza kuorodhesha Chaguzi zako katika karatasi nirahisi Sana kujua chaguo lako bora ni lipi maana katika maandishi utaweza kufikilia vizuri Zaid kuliko Chaguzi zako zikiwa kichwani tu. Ziandike kuanzia Yenye unafuuu mdogo mpaka Yenye unafuuu mkubwa Kisha chagua

4.Usifikilie Sana (Don't Overthink), Ukiona unafikilia Sana juu ya Chaguzi zako jua ipo kwenye hatari kubwa Sana maana katika maisha yetu yakilasiku tunajua vitu vyenye unafuu kwetu na visivyokuwa na faida hata likiwa suala la uchaguzi haliwez kuumiza Sana akili Zetu ila Ukiona unafikilia Sana jua upo hatarini.

ANGALIZO;Ukiona umeshindwa kufanya Chaguzi kabisa basi usiamue kwa pupa ni bora ukaomba msaada kwa watu wenye uzoefu mkubwa juu ya hilooo. Kumbuka katika maisha Chaguzi zote tunazozifanya niziwe nzur na kuachana na zile mbaya. Moja ya Faida ya Chaguzi Nzuri Ni inasaidia kuokoa muda katika mambo mengi, Lazima uyaone mafanikio ya haraka kama utachagua vizuri na kukufanya ujione mtu mwenye Bahati Sana katika maisha yako sababu Chaguzi ndio zinatueleza sisi ni Nani na nini tunafanya so choose wisely for the better future

Bahati na Chaguzi (Luck and Choices) ni vitu ambavyo vinaenda sambamba kama utafanya Chaguzi mbaya sahau kabisa kitu kinachoitwa Bahati na Kama ukichagua vizuri hivyo tambua utakuwa mtu mwenye Bahati Sana katika kila jambo unalolifanya.
Imeandikwa na [emoji1659]

Mimi Davis Abely Nziku DNA[emoji1659](22)
0755386540
 
Upvote 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…