Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. LUCY JOHN SABU KATIKA KILELE CHA WIKI YA CHIPUKIZI CCM MKOA WA SIMIYU
Mbunge wa Viti Maalum Kundi la Vijana Mkoa wa Simiyu Mhe. Lucy John Sabu katika kilele cha Wiki ya Chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu yaliyofanyika kimakoa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Sabu alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho.
Kilele hicho cha maadhimisho kiliambatana na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na michezo kama Mpira wa Miguu na Mchezo wa mbio za Magunia huku vijana wengi wa Mkoa wa Simiyu wakijitokeza kushiriki katika michezo na kuonyesha uwezo wa vipaji walivyonavyo.
Mhe. Lucy Sabu alipata nafasi ya kuongea na vijana hao wa Chipukizi CCM wa Bariadi na Simiyu yote aliwasisitiza kuendelea kuipenda nchi yao, kuwekeza katika masomo, kuwatii wazazi, kukipenda Chama Cha Mapinduzi na kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya, Katibu UVCCM Mkoa wa Simiyu Ndugu Athuman S. Salaga na Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Bariadi Ndugu Tinana Masanja nao walipata nafasi ya kuhutubia vijana wa Chipukizi.
#AlipoMamaVijanaTupo
#ChamaImara
#CCMImetimia
#KaziIendelee