Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Lucy Lameck amezaliwa huko mkoani Kilimanjaro mnamo mwaka 1934, alikuwa Mwanamke msomi ndani ya TANU, aliyehimu Vyuo Vikuu vya Oxford Nchini Uingereza na Michigan, Marekani
Alikuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Uwaziri Serikalini na kwa mara ya kwanza aliingia Bunge la Tanganyika mwaka 1960 kabla ya kuchaguliwa kwenye Bunge la Tanzania mwaka 1965
Alisoma mafunzo ya Unesi na baada ya kumaliza mwaka 1950 hakutaka kufanya kazi Mfumo wa Afya wa Kikoloni wa Uingereza na badala yake alianza kufanya kazi kama Katibu Mukhtasi
Kati ya mwaka 1955 na1957, alifanya kazi ‘Kilimanjaro Native Cooperative Union, na alianza kuingia kwenye siasa akifanya kazi na TANU. Akiwa TANU alikuwa Kiongozi wa Kitengo cha Wanawake na alisanifu vazi la Kitaifa la Wanawake wa Tanganyika
Kati ya Mwaka 1962 na 1965 alikuwa Waziri wa Ushirika na Maendeleo ya Jamii ikiwa ni nafasi ya kwanza ya Uwaziri kushikwa na Mwanamke kwa Tanganyika na Tanzania
Baada ya Tanzania kuundwa ashika nafasi ya Naibu Waziri wa Ushirika na Maendeleo ya Jamii kati ya mwaka 1965 na 1970 na pia Naibu Waziri wa Afya kati ya mwaka 1967 na 1972
Akiwa amezaliwa katika familia ya wakulima, amefanya kazi maisha yake yote kuimarisha hali za Wanawake nchini hadi alipofariki Machi 1993 kutokana na Magonjwa ya Figo.
- Barabara ya Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati wa Tanzania, Lucy Lameck. Alikuwa Waziri wa 1 mwanamke wa Tanzania
- Mashujaa wa Mlima Kilimanjaro: Lucy Lameck na Yusuf Olotu