Ludovick Utouh: Sijawahi wala sitakuja kujuta kuhusu ripoti ya 2012 iliyosababisha Mawaziri 8 kujiuzulu

Ludovick Utouh: Sijawahi wala sitakuja kujuta kuhusu ripoti ya 2012 iliyosababisha Mawaziri 8 kujiuzulu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh, amesema wakati wote hajawahi kujuta na wala hatakuja kujuta katika ripoti yake ya mwaka 2012 iliyosababisha mawaziri wanane kujiuzulu.

Utouh ametoa kauli hiyo jijini Dodoma leo Oktoba 26, 2018 wakati akizungumzia masuala ya uongozi wakati wa wiki ya asasi za kiraia.

Amesema kwamba hatua ya kujiuzulu kwa mawaziri hao ilitokana na taarifa yake ambayo ilikuwa ni ya kweli bila ya kumsingizia mtu.

Amesema kitendo hicho kiliwagusa wengi na hata kumwambia kuchukua tahadhari lakini akasema aliwaza na kubaini hakuwa amemuonea mtu badala yake alijua kila mmoja analitambua hilo ndiyo maana amekuwa akiishi na kushirikiana na waliojiuzulu kama Watanzania bila ya kubaguana.

Mawaziri waliong’oka mwaka huoni baada ya ripoti yake kujadiliwa bungeni ni; Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Omary Nundu (Uchukuzi), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii) na Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii).

Wengine ni; Mustafa Mkulo (Fedha) na William Ngeleja (Nishati na Madini) na manaibu waziri wawili; Athumani Mfutakamba (Uchukuzi) na Dk Lucy Nkya (Afya).

Mstaafu huyo amesema Watanzania wengi wanafanya kazi kama watu wenye matarajio ya kudumu milele bila kujua nafasi zao walizikuta na tena wataziacha hivyo ingewapasa kufanya kazi kwa uangalifu mkubwa ili mradi wasivunje sheria za nchi.

“Watu waepuke kufanya kazi kwa mazoea, wanatakiwa kufanya kazi kikamilifu na kuwa na mawazo ya kubuni siyo kufikiri kuendeleza yaliyoachwa na watangulizi wao.”

“Lakini kingine hiki ni muhimu zaidi viongozi wengi wanakaa madarakani na kusahau kuna raia wengine au kama watakuja kurudi uraiani, lakini mpanda ngazi hushuka,” amesema Utouh.

Katika uongozi amesema kuna viongozi wengi wenye dhamana hawafanyi uamuzi hata kushauriana na walio chini yao jambo linalopelekea kukaa na mafaili kwa muda mrefu bila kuyafanyia kazi.

Amesema baadhi hata wakikaa madarakani miaka mitano wanafanya yale yale yaliyoachwa na wenzao kwani wanafanya kwa mazoea tu.

Aliwataka kuwa na tabia ya kuwashirikisha watu wa chini yao na kutoa nafasi ya kuwasikiliza kwani uongozi ni jalala hivyo lazima kupokea zaidi na kuyafanyia kazi kwani baadhi ya mawazo yanakuwa ni mazuri.

Katika hatua nyingine amewataka viongozi kutambua kuwa wamepewa dhamana ya kuongoza wao si familia zao hivyo mtu akipewa nafasi yoyote hata kama ni urais au nafasi nyingine za juu wasiruhusu uongozi wa familia bali uongozi unakuwa ni taasisi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kila linalosemwa ni la kweli
Tumepigwa Richmond ni kweli Tena na lowasa
Tumevutishwa unga club billican ni kweli Tena na mbowe
Tumepigwa kwenye vitalu na nyalandu
Tumeibiwa ardhi yetu Tena na sumaye
 
Kila linalosemwa ni la kweli
Tumepigwa Richmond ni kweli Tena na lowasa
Tumevutishwa unga club billican ni kweli Tena na mbowe
Tumepigwa kwenye vitalu na nyalandu
Tumeibiwa ardhi yetu Tena na sumaye
Chenge/ ngeleja/Tibaijuka.....mchumia tumbo wakati wote ni siasa hata pale ukweli unapotamalaki!...Ccm ndio wanaongoza nnchi na ma scandal....mengi ni wao..ila wewe unafikiri wachache waliohamia upinzani wamehama na scandal......akili ndogo....
 
Mpaka hii Awamu itoke madarakani nchi hii itakuwa imerudi kule kwenye miezi 18 ya Nyerere ya kufunga mikanda iliyogeuka kuwa miaka karibu 10 ya mateso kwa wananchi. Hiyo ilikuwa baada ya vita na Uganda lakini hii itakuwa baada ya wananchi kumtupilia mbali Magufuli toka madarakani.
 
Back
Top Bottom