Lugha chafu, dharau na rushwa kwenye huduma za kijamii, hospitali, idara ya maji, TANESCO na ofisi nyingine za Serikali hata hili serikali mshindwa?

Lugha chafu, dharau na rushwa kwenye huduma za kijamii, hospitali, idara ya maji, TANESCO na ofisi nyingine za Serikali hata hili serikali mshindwa?

ryan riz

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
423
Reaction score
683
Kwanini haya masuala yamerudi kwa kasi kwa hawa watoa huduma?

Mbona mengine hata hayaitaji fedha kutasimamia lakini wananchi wanakumbana na hii janga la kudharauriwa, kunyanyapaliwa, kukejeli, kutojaliwa na wala kutoheshimiwa... na ukitaka ukwepe hayo yote basi TOA RUSHWA..

Tunaenda wapi sasa kama nchi, mbona watumishi ni wale wale ambao kuna kipindi walionekana wameanza kustaarabika?
 
Wafanyakazi ofisi nyingi za umma wana madeni ya mikopo bank, mitaani kwa riba umiza na saccos. Kwa kifupi muda wote wameishiwa na wanawaza jinsi ya kumwibia mwajiri iwe kwa per diem, overtime au allowance za kiwizi wizi. Ndiyo maana najibu ya shobo kwa wateja hayawakauki mdomo

Inabidinuwaelewe tu
 
Ule uwajibikaji wa wakuu wa vitengo kutoka nje yaa ofisi zao na kuacha kukalia viti kuangalia namna huduma inavyotolewa kwa wanaowangoza,na pia kuuliza wananchi km wameshapata huduma? UMEPOTELEA WAPI UWAJIBIKAJI HUU?
 
Kwanini haya masuala yamerudi kwa kasi kwa hawa watoa huduma...?

Mbona mengine hata hayaitaji fedha kutasimamia lakini wananchi wanakumbana na hii janga la kudharauriwa,kunyanyapaliwa,kukejeli,kutojaliwa na wala kutoheshimiwa... na ukitaka ukwepe hayo yote basi TOA RUSHWA..

Tunaenda wapi sasa km nchi,mbona watumishi ni wale wale ambao kuna kipindi walionekana wameanza kustaarabika..?
Jiwe hakuimarisha mifumo ya uongozi, alikuwa ni one man show! Alijijenga yeye tu! Hivyo hali imerudi vile kwa kuwa na hili mkalitazame pia!
 
Kuna mambo huwa yanafurahisha sana. Kwa hiyo mleta uzi;-
- Huwa unaenda maofisini kupata huduma zako unazozihitaji au huwa unakuwa mpelekezi kwa muda juu ya mienendo ya watumishi?

  • Unapendelea waweje kinuonekano?Wachekecheke muda wote au upate huduma na kushika kiguu na njia?
  • Unapotoa takwimu kwa kujumlisha ofisi zote,ina maana umeingia ofisi zoooteee Tanzania bara na visiwani Zanzibar na Pemba?

- Huwa unaacha kudai huduma na kubaki kuwakazia sura watumishi uone miitikio yao kwa kadiri ya heshima, upole, uharaka, ubora na ufanisi utolewao?
 
Chukua sheria mkononi watwangwe tu hadi akili zikae sawa,wasipo jifunza tuwafundishe.
 
Tuacheni mama anaupiga mwingi[emoji3][emoji3]
Siku akija mitaa na kujionea kinachoendelea au kukisikia anaweza vunja baraza la mawaziri na kutimua makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa idara nyingi sana
 
Mama alisema hivi na hapa namnukuu: .."nidhamu kwa watumishi iliyokuwepo awamu ya Tano ilikuwa nidhamu ya woga, Mimi nataka watumishi wawe na nidhamu yao ya asili bila kuogopa Simba wa Yuda..."
Kwahiyo mkuu mleta mada huko alipo mama anafurahi sana kuona watumishi wakiwa katika nidhamu gao " natural!
Na bado tu, subiri muone matokeo ya form four ya shule za umma maana ya darasa la saba tumeyaona!
 
Kuna mambo huwa yanafurahisha sana.Kwa hiyo mleta uzi;-
-huwa unaenda maofisini kupata huduma zako unazozihitaji au huwa unakuwa mpelekezi kwa muda juu ya mienendo ya watumishi?
-unapendelea waweje kinuonekano?Wachekecheke muda wote au upate huduma na kushika kiguu na njia?
-unapotoa takwimu kwa kujumlisha ofisi zote,ina maana umeingia ofisi zoooteee Tanzania bara na visiwani Zanzibar na Pemba?
-huwa unaacha kudai huduma na kubaki kuwakazia sura watumishi uone miitikio yao kwa kadiri ya heshima,upole,uharaka,ubora na ufanisi utolewao?vvv
Je utoaji wa huduma bora unaweza fanyika kwa kificho?
Utoaji wa huduma bora ni lazima mfanyakazi acheke cheke?

Usichojua ni kwamba UKARIMU katika huduma ni moja ya vigezo vya KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI..
Kingine usichokijua urasimu huchangiwa kwa kiasi kikubwa uwepo wa huduma mbovu katika taasisi husika..wananchi huona kwamba ili mambo yaende basi lazma atoe kitu(rushwa)

Suala la unajuaje au sijui umetembelea ofisi zote nchini( hapo upeo wa akili unaonesha we ni nani hivyo siwezi kubishana na wewe,sababu kila mtu anakazi yake)
 
Usipojua matumizi ya tafadhali, samahani, boss, mkuu, kaka, dada, mama, mwananchi, au mwanasimba, nk, wewe unapandisha kibesi utaona stress za hao watumishi wanamalizia kwako.

Unakuta limtu hata halijakusalimia linauliza, nimemkuta mkuu, nalijibu tu kamtafute.
 
Je utoaji wa huduma bora unaweza fanyika kwa kificho?
Utoaji wa huduma bora ni lazima mfanyakazi acheke cheke?

Usichojua ni kwamba UKARIMU katika huduma ni moja ya vigezo vya KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI..
Kingine usichokijua urasimu huchangiwa kwa kiasi kikubwa uwepo wa huduma mbovu katika taasisi husika..wananchi huona kwamba ili mambo yaende basi lazma atoe kitu(rushwa)

Suala la unajuaje au sijui umetembelea ofisi zote nchini( hapo upeo wa akili unaonesha we ni nani hivyo siwezi kubishana na wewe,sababu kila mtu anakazi yake)
Unajibu maswali kihuni na kujifichaficha sana.Punguza au ikibidi uache chuki zako kwa watumishi.Hamkosi kuzua mambo ninyi!Waacheni wafanye kazi kwa kujiamini.Mkifika maofisini mnatafuta la kutoka nalo kwa u-hasihasi tu.Zama za watumishi kufanya kazi kama wapo medieval ages zimepita.
 
Kiuhalisia biashara ya kutoa huduma watanzania limetushinda. Iwe kwenye taasisi za umma ama binafsi,limetushinda.
 
WaTanzania wengi ni hawana maadili mazuri. Hawaezi kuwajibika kwa haki bila kuwasimamia.

Hapo hao ni wale wanakesha makanisani kusali siku za wiki na jumapili, wanakesha miskitini muda wote kuswali lakini tabia na maadili ni mabaya.
Majizi, wavivu, kutowajibika, rushwa, kiburi, jeuri, dharau, unafiki, lugha chafu na mengine mengi ya hovyo.

Miskitini na makanisani wanaenda kufanya nini?

Hivyo lazima kuwasimamia muda wote au sheria kali zitungwe kuwadhibiti hawa watu.
Kuanzia mitaani hadi jumba jeupe hali ni hivi hivi tu.
Wengine wanakuambia kabisa tusiibe, tuache rushwa inakuaje kule juu wala rushwa!
 
Kwanini haya masuala yamerudi kwa kasi kwa hawa watoa huduma?

Mbona mengine hata hayaitaji fedha kutasimamia lakini wananchi wanakumbana na hii janga la kudharauriwa, kunyanyapaliwa, kukejeli, kutojaliwa na wala kutoheshimiwa... na ukitaka ukwepe hayo yote basi TOA RUSHWA..

Tunaenda wapi sasa kama nchi, mbona watumishi ni wale wale ambao kuna kipindi walionekana wameanza kustaarabika?
Nilishasema na ninasema tena mbona hamuwi specific kuwa ni ofisi gani na ikibidi jina la mtumishi mwenye mwenye mwenendo usiofaa au uliokukera.? Msiseme kijumla jumla hivi kwani inaonekana kama ni umbea tu na uzushi.Wapo watumishi wa umma wenye uadilifu na wanaotoa huduma kwa viwango vya juu pasipo kudai rushwa wala kutengeneza mazingira ya rushwa.Nasema wapo tena sio kidogo, wapo.Fake ID ikufanye basi kuongea kwa uwazi, kwani gharama anayoilipa Maxcence Mello ni kubwa sana kwa kutofichua real ID za members huku halafu mtu unakuja na umbea badala ya ushahidi.
 
Tatizo hatuna kauli nzuri hata kama ile ni ofisi ya uma ila wahudumu ni binadamu waatu wengi wanalalamika sjui rushwa sjui kauli chafu mbona mm sijawah kutana na hzo kero hata siku moja
 
Jiwe hakuimarisha mifumo ya uongozi, alikuwa ni one man show! Alijijenga yeye tu! Hivyo hali imerudi vile kwa kuwa na hili mkalitazame pia!
Wewe ndo mjinga, kwani huwezi kutekeleza wajibu wako hadi jiwe awepo? Kuna watu wa hovyo sana wanafanya upumbavu wanasingizia eti jiwe alikuwa one man show.
 
Back
Top Bottom