Ingelikuwa vyema tuendelee na tofauti zetu ila tujifunze kuishi nazo na kuishi na watu wenye lugha tofauti, tamaduni tofauti na mitazamo tofauti
Ni wazo zuri makyao. Lakini nani atakubali kuacha lugha yake akumbatie ya mwenzie?
Pia ingekuwa vema ukitoa mapendekezo ya namna ya kuanzisha hiyo lugha na namna ya kumfikishia kila binadamu wa kila sehemu. Mfano, tukichukua kichagga kiwe lugha hiyo, tunaanzia wapi?
Dunia ya sasa inataka mtu ajue lugha nyingi awezavyo.Kwamba ULIMWENGU unaweza kukubaliana kuwe na lugha moja tu... kwa maoni yangu naona itakuwa ngumu.... chukulia mfano wafaransa walivyo na kiburi na lugha yao.Ukienda kwao hata kama wanajua kiingereza, ukiwasemesha hawatajali kukujibu..inabidi uanze kutafuta vocabulaire yako iliyopotea miaka mingi uweze angalua kuomba maji.Lugha ni utambulisho - mara nyingi lugha zilizokomaa, wenyewe hawatapenda kuzipoteza na watazilinda kwa gharama yoyote ile.Hapa Tanzania kuna mapambano kutaka kukipandisha kiswahili kwenye chati zaidi ili angalau kiwe moja ya lugha zenye kutumika angalau kwenye bara la Africa....jitihada hizi haziko kwenye kiswahili tu, ziko pia kwenye lugha nyingine kama kihausa n.k. Mwelekeo nionavyo hauko katika kupata lugha moja bali kueneza lugha nyingi zaidi ulimwenguni.
BLURAY,
Hitimisho lako linanitia wasiwasi.
Je ni lazima A akishindwa na B ashindwe?
Unataka kutuambia kuwa kabla ya mnara wa babel lugha ya dunia ilikuwa moja!?Toka mwanzo ilikuwa ni makusudio ya Mungu dunia iwe na mchanganyiko wa lugha (waaminio biblia watakubaliana nami), mfano mzuri ni pale Mungu alipomwambia Ibrahim wakti ule hana mtoto, alimwambia kuwa usisikitike nitakufanya kuwa baba wa mataifa (na ili kuwe na mataifa lazima kuwe na tofauti ya utamaduni, na lugha ni sehemu ya utamaduni), lakini kuon esha ubaya wa kuwa na lugha moja dunia nzima, hebu turejee hadithi ya Mnara wa Babeli.
Hili lilishajaribiwa na lugha ya Esperanto ambayo ilishindwa vibaya sana, it is not practical at all.Ukitaka kujifunza how impractical this is study the fall of Esperanto.
Je, ulifuata shauri lako? Ulifanya utafiti kuhusu "the fall of" Kiesperanto? Kwa nini unaazima kwamba lugha ya Kiesperanto ilishindwa "vibaya sana"? Mimi mwenyewe naongea Kiesperanto pamoja na watu wengi ulimwenguni. Tafadhali soma zaidi (www.afriko.org)!
Lugha ya Kiingereza ni lugha ya ukoloni mamboleo.
Kiesperanto, lugha iliyokuwa na aspiration ya kuwa lugha ya dunia, mpaka leo inaongewa na watu wangapi?
..............................Mbona unataka kukipa chati wakati hata wanaoongea kisukuma ni wengi zaidi? .