Lugha ya ishara kuwa lugha rasmi DRC

Lugha ya ishara kuwa lugha rasmi DRC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepanga kuiweka lugha ya ishara kuwa lugha ya tano rasmi nchini humo ukiongeza kwenye Kiswahili, kilingala, Kituba na Tshiluba.

Lugha hiyo ya ishara itakuwa inafundishwa shuleni ili kuwasaidia watu ambao wanategemea lugha ya ishara kupata huduma za serikali kwa urahisi.

"Ni jamii ambayo kwa muda mrefu imekuwa haipewi kipaumbele kwasababu ya changamoto ya mawasiliano," waziri wa walemavu nchini humo, Irene Esambo, ameiambia BBC.

Kumekuwa na kesi za watu kufa wakati wakitafuta tiba kwasababu tu hawakuweza kujieleza na wengine walishindwa kesi mahakamani kwa sababu ya kushindwa kuwasiliana, kwa mujibu wa mwalimu wa lugha ya ishara Nicola Tshilomba.

Wataalamu wa lugha za ishara kutoka majimbo mbalimbali nchini humo wako katika kikao kwa siku 30 ili kukubaliana mfumo mmoja wa kufundisha lugha hiyo mashuleni.

Serikali ina mpango wa kuzindua kamusi ya lugha ya ishara.

DRC inakadiriwa kuwa na watu milioni mbili ambao wana ulemavu wa kuona na kusikia ,kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya duniani ya mwaka 2012 .
 
Back
Top Bottom