Lugha ya kabila gani ikiongelewa uwa una furahia sana?

Lugha ya kabila gani ikiongelewa uwa una furahia sana?

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,221
Mimi binafsi si msambaa Ila hawa jamaa wakiongeaga lugha yao Huwa naenjoy sana hususani zile lafudhi zao kama vile hela wanaita hea, nyumbani wanaita nyumbai.

Kabila lingine ni wamakonde wakiongea kilugha chao Huwa naenjoy sana yaani naburudika napenda sana kuwasikiliza.

Na kabila la mwisho ni wamwera na watu wa kusini Kwa ujumla mtwara na wanapoongea Kiswahili chao kilichochanganyika na kilungha yaani hata mtwara wanaita ntwara,mtu Mambo anasema ntu [emoji1787][emoji1787]

Wew kabila gani linakushangaza na kukufurahisha wanapoongea lugha yao au kiswahili.
 
Waganda naenjoy sana wakiongea !
 
Mi msambaa ila napenda wadigo wanavyoongea na wapemba Kwa sababu nimekaa nao sana.

Wasambaa wanakaza ulimi na meno yaani akiongea anatumia nguvu sana... Wadigo na wapemba wanaongea bila ya jazba bila hata mtu awe na hasira unaweza fikiria yupo kweny mood ya kawaida.

wairaq ,wapare na wamasai wananikera kupenda kusunya Kwa kutumia koo yaani unasikia sauti kweny koo ,ujue hapo mtu kakasirika ..Wapare utasikia "khaaarikha'
 
sijawahi kusikia wazaramo wakiongea lugha yao
 
sijawahi kusikia wazaramo wakiongea lugha yao
Wazaramo, wapemba , Wadigo ,wandengereko ni nadra sana kuwakuta wanaongea kikabila...Na hata wakiongea maneno Yao mengi yapo wazi yanaendana na kiswahili.
 
Back
Top Bottom