SoC04 Lugha ya Kiingereza itumike kufundishia na kujifunza kuanzia awali mpaka chuo kikuu

SoC04 Lugha ya Kiingereza itumike kufundishia na kujifunza kuanzia awali mpaka chuo kikuu

Tanzania Tuitakayo competition threads

bigamboc7

New Member
Joined
May 23, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Tanzania tuitakayo lazima iwe na raia walio wengi Kwa ulimwengu wa sasa ambao angalau wawe na uwezo wa kutumia lugha za kimataifa angalau hata lugha moja ambayo itawawezesha kujiimarisha kiuchumi(Biashara za kimataifa), kisiasa (kitaifa na kimataifa), Sayansi na tekinoogia ( ambayo sasa Dunia inawekeza nguvu, rasilimali pesa na watu kwenye tekinoogia), na kadhalika. Sasa ili haya yote yaweze kufanikiwa Kwa ufanisi mkubwa lazima lugha ya Kiingereza itiliwe mkazo kuanzia AWALI MPAKA CHUO KIKUU Kwa sababu kuu zifuatazo.

Kupata maarifa kwenye internet. Watanzania walio wengi wanashindwa kupata maarifa mbali mbali kutoka kwenye vyanzo mbali mbali kwenye internet kwasababu vyanzo vilivyo vingi vimeandikwa Kwa lugha ya Kiingereza,mfano makala zilizo nyingi, vitabu vilivyo vingi vimesheheni maarifa tofauti tofauti na mengi ambayo pengine huwezi kuyapata Kwa walimu wanaotumia Kiswahili.

Lakini vile vile kuna walumu wengi kutoka maarifa mbali mbali ambao wanapatikana kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, YouTube Twitter na kadhalika, lakini hawa walimu walio wengi wanaotumia lugha ya Kiingereza kufundishia.

Kwa mtanzania wa kawaida aliye ishia darasa la Saba na form four wakuwa wanakosa fursa hii ya kielimu kutokana Kwamba wao lugha ya Kiingereza nitatizo hawaielewi. Lakini huyu mtanzania angefundishwa lugha hii tangu awali basi maarifa haya ngeyapata kikamilifu kwenye internet.

Kufundishia mtandaoni.Watanzania walio wengi wana maarifa yao wenyewe ambayo wanapaswa walimwengu wote wajifunze kutoka kwao. Ambavyo walitakiwa hayo maarifa( maudhui) wayauze kwenye internet kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, YouTube, Instagram, Pinterest, WhatsApp na kadhalika, kinachowakwamisha watanzania walio wengi nikwamba umma wa watu walimwengu mtandaoni( internet) wanakifiwa Kwa kuwasiliana Kwa lugha ya Kiingereza. Ambavyo sasa Kwa mtanzania ni ngumu kwake, kwahiyo unakuta hawa watanzia wanakosa hii fursa ya kufundisha mtandaoni ili wajiingizie kupata Kwa sababu tu ya kukosa msingi mzuri wa lugha ya Kiingereza kipindi alipokuwa shuleni.

Kupandisha ufaulu wa elimu ya sekondari na ngazi za elimu zingine zinazo fuata. Jinsi mjuavyo tangu na tangu katika matokeo ya elimu ya sekondari somo la Kiswahili nimekuwa ni kinara Kwa ufaulu. Siyo kwamba ni rahisi hapana ni kwasababu tu wanafunzi walio wengi ni wazungumzaji wa Kiswahili Kwa ufasaha kuliko Kiingereza ndiyo maana wanamwelewa Mwaimu na wanalifaulu somo Hilo Kwa wingi.

Masomo mengine yaliyo baki yanatumia lugha ya Kiingereza na wanafunzi walio wengi wanayafeli, nikwasababu huyu mwanafunzi huko elimu ya awali na msingi alisoma Kiingereza kama somo na siyo lugha ya kujifunzia na kufundishia.

Sasa anapokuja sekondari anakuta mambo ni kinyume ambavyo Kiswahili ni kama somo alafu lugha ya kujifunzia ni Kiingereza na vitabu vya masomo yote vimeandikwa kwa Kiingereza isopokuwa vya somo la Kiswahili, sasa huyu mwanafunzi unakuta huyu mwanafunzi anachanganyikiwa Kwanza ajue lugha ya Kiingereza alafu ayajue masomo, kwahiyo anaishia kufeli. Lakini kama huyu mwanafunzi angekuwa ameizoea lugha ya Kiingereza kama Kiswahili basi hivyo masomo mengine pia angeyafaulu kama ilivyo kwenye somo la Kiswahili na hatimae ufaulu katika elimu ya sekondari angekuwa juu.

Kukuza utalii. Kama mnavyo fahamu kuwa Tanzania inavivutio vingi vya watalii barani Africa, lakini kuna inchi nyingi Afrika hazina vivutio vingi vya watalii kama vya Tanzia lakini hizo inchi ndiyo zinaongozwa kutembeleawa na watalii wengi kuliko Tanzania.

Hii yote nikwasababu siku hizi masomo ya utalii yamehamia mtandaoni ( Internet) sasa ili yaweze kuwafikia jamii ya internet ambayo jamii hii inawasiliana Kwa lugha ya Kiingereza, basi hayo matangazo pia ya utalii yanabidi yawekwe Kwa Kiingereza ili yawafikie watu wengi na wawezekuvitembelea vivutio vyetu vya utalii. Kwa watanzania inakuwa ni vigumu Kwasababu watanzania walio wengi wanashindwa kuweka matangazo hayo Kwa lugha ya Kiingereza ili kuwafikia watu wengi Zaidi.

Kuchangamkia fursa mbali mbali Dunia. Duniani kunafurusa mbali mbali ambao zinajitokeza Kwa vijana wakiafrica, Kwa mfano fursa za kimasomo, mashindano mbali mbali,tehama, ajira na kadhalika, vijana wengi wakitanzania fursa hizi zinawapita au wanziogopa siyo kwamba hawawezi nikwasababu unakuta katika hizo fursa lugha itumiwayo nikiingereza, ambavyo Kwa kijana wakitanzania hayuko mahiri katika lugha hii. Lakini kama lugha hii huyu mtanzania angeitumia kuanzia ngazi ya awali mpka CHUO KIKUU huyu mtanzania anglikuwa mahiri na fursa nyingi za duniani angeshiriki kikamilifu.

Kufundisha lugha ya Kiswahili Kwa maarifa ya kigeni duniani. Ni ukweki usiopingika kuwa maarifa yasiyo tumia lugha ya Kiswahili wanahitaji walimu wa Kiswahili ili waweze kuwafundisha raia wao Kiswahili.

Sasa ili mwalimu aweze kuelewana na wanafunzi wake inabidi yeye Mwalimu awe anaifahamu lugha yao Kwa ufasaha, mfano wanafunzi wanajua Kiingereza mwalimu pia inabidi awe anaifahamu lugha ya Kiingereza ili yeye awafundishe Kiswahili Kwa ufasaha. Lakini sasa Kwa watanzania walio wengi niitofauti kwani wao wanajua tu Kiswahili kwo unakuta hii fursa ya kufundisha Kiswahili kwa watanzania inapotea kisa tu hawajui lugha za kimataifa kama Kiingereza au kifaransa ili waweze kukitumia kuwafundisha raia WA kigeni.

Hivyo naihasa serikali kuweza kufatilia upya matumizi ya lugha ya Kiingereza shule zote za serikali hasa hasa shule za msingi na awali ili wanafunzi waweze kujengewa uwezo wa kujieleza Kwa Kiingereza katika mazingira tofauti tofauti ambayo yatamnufaisha mtu mmoja mmoja.

Na hiyo ndiyo Tanzania tuitakayo.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom