Lugha ya Kiitaliano

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Kiingereza, kifaransa, kiarabu, na kiispania ndio lugha zinazo zungumzwa na watu katika nchi nyingi duniani. Kiingereza karibu makoloni yake yote ndio lugha wanayotumia, hali kadhalika kwa kifaransa hivyo hivyo. Kiispania kinapatikana huko america kusini na kaskazini kwa kiasi kikubwa. Kireno nacho kipo kwenye nchi chache hapa afrika na kule kusini amerika. Kijerumani kipo pale ulaya kwenye nchi ya Austia.

Hoja hapa, nimavyojua nchi za Ureno, Italia na spain watu wake ni walatino. Italy lugha yake inazungumzwa na nchi gani nyingine hapa duniani? Hivi hamna lugha ya kilatino? Au kilatini ndio kispanyola/kireno au kitaliano?

 
Kitaliano ndo kilatini.ndo vile papaa....bruto bruto malaca flambeto,korkodio pistole mayale....
 
Kitaliano ndo kilatini.ndo vile papaa....bruto bruto malaca flambeto,korkodio pistole mayale....

kuacha italy nchi gani tena inatumia hiyo lugha. Ujue hii ni moja ya lugha kongwe kabisa duniani.
 
kwa kifupi mlomlongo wa nchi zifuatazo huzungumza kwa kiasi ainishwa ktk mlolongo
 

Attachments

  • italiano.PNG
    13.5 KB · Views: 199
Sijui sana, lakini ninavyojua mimi, kilatino na kiitaliano ni lugha mbili tofauti kabisa. Mpaka kufikia hii leo wanasema kilatin does not exist any more. Ninamaana hakuna watu waliobaki/waliokuwepo mpaka sasa wanaowasiliana kupitia hii. Nimekutan na watu wachahe ambao wanasema walisoma latin in school, lakini hawakufundishwa full grammar kama lugha nyingine, wanasema walionyeshwa few frases tu. Yaani kuna few sentences maarufu sana ndio zinatumika sana.
Lakini kuna lugha nyingi za wazungu zimetoka na na latin languge, ndo maana kwa kiasi kikubwa hawa watu wanasikilizana sana japo si kwa 100%. Kwa mfano mimi ninajua kuongea,kusoma na kuandika español, lakini naweza kusikiliza maongezi ya portuguese au italiano na kuelewa kila kitu,kitakachonishinda ni matamshi tu.
Si español,italiano na portuguese na italiano tu, kuna lugha nyingine kama za Rumania,ex-Yugoslavia, Hungary e.t.c zote ni za karibu sana na latin language. Lakini ukichunguza sana utakutana na latin language hata kwenye kiingereza, kifaransa na lugha nyingine. Sina uhakika na dutch au germany lakini for ure kuna maneno mengi tu ya kilatino.
 
KITALIANO ni lugha rasmi nchini Italia na Uswisi (hawa wana lugha kuu 3-kijerumani, kifaransa na kitaliano na ya 4 kiladino,sio kilatino, tusizichanganye ). Kuna nchi ambapo zina wakaazi wengi wenye asili ya Italia, watu hao hutumia lugha hii ingawa sio rasmi kiserikali ila hutumia baina yao wenyewe (minority language). KILATINI kwa sasa ni lugha ilokufa na hamna watu wanoizungumza 100% ila watu husomeshwa misemo na maneno tu ya lugha hii. KILATINI kimezaa KITALIANO,KIRENO,KISPANISH,KIFARANSA,KIROMANIA/KIMOLDOVA NA KIKATALAN(LUGHA YA KIKABILA YA BARCELONA NA VALENCIA, WANAZUNGUMZA HII UKIACHIA KISPANISH). Wahangari na lugha yao ipo peke yao ulaya,ila sio kilatini.EX-yugoslavia wanazungumza lugha za kislavik (zinashabihiana na kirusi) isipokiwa wakosovo ambao wao lugha yao ni Kialbania.
 
kuacha italy nchi gani tena inatumia hiyo lugha. Ujue hii ni moja ya lugha kongwe kabisa duniani.
Kitaliano kinazungumzwa italia tu kama lugha ya taifa. italy hawaongei lugha nyingine. kwingine wanakoongea hata kama sio rasmi ni Brazil, Argentina, mexico na nchi nyingine za latin amarica. latin america ni nchi ambazo kuna wahamiaji/settlers wengi sana wa kitaliano walienda enzi hiyo za ukoloni na pamoja na kwamba wanaishi kule hadi leo wanao uraia wa italy. na wanaongea kitaliano pia (kama vile walivyo wahidi hapa bongo wanaongea kihindi hadi leo pamoja na kwamba walikuja miaka mamia iliyo pita). Brazil kuna watu wa asili ya kitaliano wengi sana. Uruguay, Paraguay etc, hata yule mng'ata wenzie asili yake ni mtaliano, na wanatembelea italy mara kwa mara kama wayahudi wanavyotembelea israel. inasemekana kuwa, raia wa latin america ndoto yao kuu ya kwenda ulaya huwa sio ulaya nyingine bali tangu akiwa mdogo anaota ndoto kwenda kuzamia italy au spain. hata wacheza mpira wengi wa latin america utakuwa walianzia italy ndio wakaenda kwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…