Lugha ya Kiswahili hasara

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
2,791
Reaction score
850
Tanzania lazima ibadilishe mfumo wake wa ufundishaji kuanzia msingi ili masomo yote yafundishwe kwa Kiingereza isipokuwa Kiswahili kama majirani zetu.

Ni aibu kuwa na watoto ambao hawezi kutunga sentesi rahisi kwa lugha ya Kiingereza, katika rasimu ya Warioba aliona hilo lakini Waswahili wakakataa, leo wanakuja na visera ambavyo sio mapya,ambayo ndani ya miaka 50 wameshindwa kutekeleza,kwani hatukuwa na elimu ya kujitegemea?

Hatukuwa na shule za kilimo na ufundi? Products zao ziko wapi? Hali ya shule hizo je?

Elimu bure ni uongo na hiyo kauli inatumika kisiasa maana Tanzania haina uwezo huo maana tunachangishwa kila kitu umeme,mlinzi na taka taka zote, elimu bure maana yake ni kuwa mchango zaidi.

Ni heri ulipe na michango isiwepo na bure bure hamtaweza.
 
Sera ya Elimu iliyozinduliwa jana inataka ufundishaji uwe wa KISWAHILI tu. Kiingereza itakuwa kwa watoto wa matajiri tu sio kwa kila mtu.
 
Gor
Wazungu, Wachina na Watu wengine ambao SIYO weusi wanapoamini ya kwamba Waafrika sisi ni masokwe na tuna IQ ndogo labda huwa wana haki ya kusema hivyo kwa maana ktk Dunia hii hakuna sehemu nyingine yoyote ile ambapo binadamu huiona Lugha yake mwenyewe kuwa ndiyo adui yake!
Hakuna sehemu nyingine yoyote ile isipokuwa huku Afrika kwetu tena kwetu sisi weusi tu kwa maana Wazungu wa AK wanakitukuza Kiafrikans na Waarabu wa Afrika Kaskazini pia wanakitukuza Kiarabu
 
Last edited by a moderator:
Mabadiliko yaanzie kwako na familia yako lugha, hapo kwanza umeandika kwa kiswahili.
 
Gor
Ndugu, kwa mtu makini, akiisoma hii msg yako anaweza kujiuliza sana kama we kweli ni raia wa Tanzania!?

Cheki neno lako la mwisho! Kwa taarifa yako hakuna Mtanzania makini anayekidharau Kiswahili.

Nadhani unajichanganya sana kutumbukiza hapa suala la mjadala wa aidha ni Kiswahili au Kiingereza kitumike mashuleni.
 
Last edited by a moderator:
....kwa sasa hatuna kitu, lazima tuwe na uwezo kwanza,shida ya waswahili ni kuwa Obama akisema kwaheri basi meno njeeeeeeeeeeeeeeeee!mmeliwa.Bila english hatutakuwa na wana sayansi mwezini
 
.....ndiyo shida yenu,mmejaza wanachina,waarabu,wapakistani,wathailand,wasomali mpaka mnawapa uraia eti ni watu wa tanga,nimesahau na wahutu wa burundi 160000...mie ambaye nimezaliwa ktk juu ya ardhi hii,nimezika mababu na mababu zangu hapa sio raia.....shinda ya waswahili maana mie sio mswahili.
 
kISWAHILI kitabaki kuwa utambulisho (identity) kwa mtanzania. mwanafunzi huelewa kwakutumia lugha yake mama, hata hao wanaokidharau kiswahili, kiingereza hawakifahamu vizuri, kama kuna mtu anabisha basi mtoa mada aiweke mada yake kwa kiingereza uone. Najivunia kuwa Mtanzania, kubwa kuliko yote najivunia lugha yangu ya KISWAHILI.
 
If that is a case, vigogo warudishe watoto wao bongo ili wasome mfumo huu mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…