Habari za majukumu ndugu zangu,
Nimekuwa nikijiuliza faida ya vitendawili, ngano, methali na lugha nzima ya kiswahili kwa ujumla ni nini mpaka imekuwa lugha ya taifa? Amini usiamini lugha ya kiswahili imekuwa ni mojawapo ya sababu kubwa ya kurudisha nyuma maendeleo ya taifa letu. Ni lugha changa sana haina misamiati ya kutosha..
Inatusababisha kutokujiamini, kukosa ubunifu, upungufu wa maarifa, kutokujua dunia inataka nini kwa sasa, kutokuwa na wataalamu thabiti wenye ushindani katika soko la ajira.
Kwa mtazamo wangu bora lugha ya kiswahili ingekuwa ya pili, kiingereza iwe lugha ya kwanza. Mitaala ibadilishwe watoto waanze kufundishwa tokea shule za msingi hii itajenga taifa bora na lenye ushindani.
Asanteni