Lugha Ya Mzazi Kwa Mtoto Aliye faulu Form 4!

BIGURUBE

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2014
Posts
6,748
Reaction score
4,252
SAA 12 asubuhi.

BABA;- baba, unaamka sasa hivi au unalala lala kidogo..
MTOTO;- Hapana baba nimechoka
ntaamka saa 5 jana nilichelewa kulala nilikua naangalia PRISON BREAK season 5, kumbe michael scofied hakufa.
BABA;- Haya baba basi kuna elfu 30 nimemuachia mama ako kama utajiskia kutoka utaitumia kama nauli na mimi ntaiangalia baadae iyo season.
MTOTO;- Baba si uniachie zile funguo za rav4!!
BABA;- Haina tatizo utaenda kuchukua pale chumbani kwangu usipoziona mwambie mama ako akupe, halafu
sidhani kama hiyo pesa itakutosha kwa ajili ya mafuta upitie pale ofisini nikuongeze pesa.

SASA HII NDIO LUGHA KWA WALE WALIOPATA 4 NA 0

SAA 12 asubuhi.

BABA:- We nguruwe umelala tuu mpaka saa hizi ivi unajua bei ya hilo godoro mpuuzi wewe kazi kupata maziro tuu kwa kulala lala lione bichwa kama tofali, hebu amka unioshee gari niende kazini kenge wee.
 
[emoji125] [emoji125] [emoji23] [emoji23] [emoji122] [emoji122]
 
Du asee ni kweli dogo kapata 2 kachukia nimebembembeza nimetuma elfu sabini akanunue viwalo bado kanuna kuna mpango wa kumpeleka beach labda atacheka. Watoto wangejua wangelala macho watufurahishe hakuna kitu wangekosa.
 
Wewe unataka apate daraja la kwanza au la pili shule yenyewe Mwananyamala Kisiwani? kitabu cha Fasihi kimoja, mwalimu wa kingereza anatumia kiswahili kufundisha? Hela ya masomo ya ziada mwezi huu unatoa mwezi ujao vyuma vimekaza? wewe mshua/mdingi ukisha lipa ada ulishamaliza kazi... unashinda kwenye vijiwe vya kahawa wala hutaki kujua kama dogo kaandika au hajaandika.

Msipende kupanda mbegu juu ya majabali mkatarajia mavuno!

Aaah hata hivyo atakua kafata akili za wajomba zake (ndio mnavyosema)
 
hivi hizo shule hazinaga wanaofaulu
 
hivi hizo shule hazinaga wanaofaulu
Jaribu kuangalia matokeo yao. na huyo Genius amepata daraja la tatu na comb haijabalalnce, wacha tu tuendeleze siasa za kushadadia mambo kimtandao lakini kiukweli hali sio nzuri. (Shule yenye wanafunzi 300 ina walimu watatu) wa masomo ya sanaa...
 
Yes, Kuna Kaukweli Hapo Ulivyoandika, Wazazi Chukueni Hilo!
 
bichwa kama kenge wa madoa madoa
Yupo jamaa alikuwa na pacha yake yani pacha yake kafaulu hadi akawa anatolewa vyombo na wazazi lakn yy alikuwa akikosea kitu ambacho ni lazima utakosea nikulalamikiwa mpk akawa anaomba pacha yake afeli ili aone utamu wa after school life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…