Wachina ni tofauti na wazungu, wachina wanauza bidhaa kama simu na kutafuta mali ghafi kwenye nchi zingine ni wao wa kujifunza hizo lugha husika. Wazungu wamejikita kwenye mambo ya utafiti na masuala ya demokrasia na utawala bora, kwa kupitia wazungu, wasomi wetu wanapata ajira kwenye miradi ya utafiti na serikali pia wanachota hela kwa wazungu kupitia masuala ya utawala bora na demokrasia. Ukichunguza kwa makini utagundua 95% ya wasomi wetu hujipatia mkate wao kupitia wazungu kwenye miradi mbalimbali iwe NGO au utafiti. Pia kumbuka wanachangia bajeti za serikali zetu za kiafrika na hata vyama vya siasa. Mchina kajikita zaidi kwenye biashara.