Lugha za mtaani

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Lugha za mtaani/kitaa au maskani.


Mpige tero-Msachi/mkague.
Njiti-Shilingi 100
Bati -sh 200
Barida-( tuliza/tulizana)
Chali-vijana wadogo wadogo wanaolingana umri
Nyoka-dogo ambaye hajafikia umri wa ujana(unaweza kumwambia
niaje nyoka wangu)
Mwana-Msela,mshikaji
Moko-moja
Dedisha-ua
muza-poa
sijakudere-sijakuona
Ngawira-pesa
Masai mmoja-Elfu kumi
Cha orkokola-bangi,ganja,ndumu
sedere full-usalama,shwari
haina daz-haina noma
haina gwera-iko poa
Mzuka ile mbaya-iko poa(hiyo mbaya sijui inawekwaje wakati mtu anamaanisha mambo mazuri)
acha usoro-acha ujinga
Ngoto-bastola
ndichi-ndani
dongo-ugoro
ni mori-ni safi
kutoa lock-kunywa pombe
kausha-nyamaza
vunga-acha
ngeta/roba-kaba
duku mtiti-imekolea sana
mlupo-msichana malaya
kiraruraru-kimbelembele
hakuna shobo-hakuna tatizo
CHADEMA-mia mbili(nadhani mia mbili inaitwa chadema kwa vile chadema wanaonyesha vidole viwili)

Unaweza kuongeza lugha zingine za mtaani au kitaani kwako,hizi zinatumiaka sana Arusha(Arachuga)
 
kauzibe

Tantalila

michosho

chabo

unyunyu

mwake

mwela

wese

mwani

asteaste

mtanange

gundu

ng'ana/ndumu

gozi gozi

mwana/mwanangu

mpelampela

mbwisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…