Lugha za vijiweni zitumiwazo na baadhi ya wabunge zinakera sana

Lugha za vijiweni zitumiwazo na baadhi ya wabunge zinakera sana

SundayM

New Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2
Reaction score
2
Kama mfuatiliaji mzuri wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania utaungana nami kuwa baadhi ya wabunge wamesahau majukumu yao na kulifanya bunge kama kijiwe cha mabarobaro amboa kwao lugha za( umebugi men,baridaa,mizinguo,kumpa makavu,tutazinguana...na n.k) ni za kawaida na ndio huona zinawafaa kwa rika lao, lakini sasa hivi lugha hizi zimeingia bungeni na baadhi ya wabunge hujiona wanakwenda sana na wakati pindi watumiapo maneno haya ya kihuni,kwa ukweli hali hii inasikitisha sana,kama wanafikiri kwamba hivyo ndiyo namna ya kuwawakilisha vijana basi wajue huo si msingi wa maadili katika taifa hili.Pia watambue kuwakilisha vijana ni kutatua matatizo yao ambao wao kama wawakilishi wao wanapaswa kuwajibika kwa hilo na sio kupoteza muda na pesa za walipa kodi kwa kuleta lugha za vijiweni,kama katika fikra zao hakuna matatizo ya wananchi basi warudi majimboni wakaone then wakayawakilishe....
 
Back
Top Bottom