Naskia hao BRTSH CONC. wanamkasi mrefu ( tuition fee)[/QUOTE]
ukiogopa 'mkasi' rafiki yangu unaweza usifikie lengo lako. Mambo mazuri yana gharama. Hizi kozi za bei rahisi nyingi "za kichina". Napenda pia kukushauri kuwa, wakati au baada ya kupiga kozi yako, jiweke ktk mazingira flani yatakayokufanya upongeponge ung'eng'e. Kwa mfano, tazama movies zenye 'subtitles' za english, soma novels, cheki media inayotangaza news kwa kiingereza kama BBC, CNN, DWTV n.k. Pia soma magazeti kama The Guardian, Sunday News n.k. Katika mambo hayo yote, usisahau kuwa mdadisi. Ukikutana na msamiati usiouelewa, jaribu kuulizauliza kwa wakali wa haya mambo. La mwisho, tafuta dictionary au kama unayo that's great! Napendekeza uwe na ile 'Oxford Advanced Learners' kubwa ya English-English. Good luck!