Luhaga Mpina ampongeza Rais Samia kasi ya Ujenzi wa Miradi, asema hakuna ambao unasuasua

Luhaga Mpina ampongeza Rais Samia kasi ya Ujenzi wa Miradi, asema hakuna ambao unasuasua

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
390
Reaction score
385
LUHAGA MPINA AMSIFU BUNGENI MH. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KASI NZURI YA UJENZI MIRADI YA SGR KIPANDE CHA MWANZA- ISAKA NA MIRADI YA TARURA

"Mhe. Spika na mimi nashukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia wizara hii muhimu sana, wizara ambayo inatunza rasilimali za W atanzania.

Na niseme kwanza nampongeza sana Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi anavyoendelea kwamba mpaka sasa hivi hatuna mradi wowote ule ambao unasuasua.

Miradi yetu ya kimkakati yote inaendelea vizuri, Certificate zote zinalipwa kwa wakati kwa hiyo ni pongezi kubwa sana kwa Mheshimiwa Rais wetu lakini zaidi pia kwa kutenga fedha bilioni 372.6 kwa ajili ya kipande cha Isaka- Mwanza cha SGR na kama hiyo haitoshi kwa kutoa fedha bilioni 187 ku support TARURA kupata miradi ambapo kila jimbo limepelekewa Milioni 500 na mimi za jimbo langu nimeshataarifiwa zimeshafika na mipango kule inaendelea vizuri.

*#BUNGENI LUHAGA MPINA# BAJETI WIZARA YA FEDHA 7.6.2021 # PONGEZI KWA MH. SAMIA SULUHU

IMG-20210609-WA0191.jpg
 
Ile rula yake ya kupimia samaki ipo?
 
Naona sasa amechoka kupigania legacy ya mwendazake. Akili zake sasa zimerejea baada ya kushikiwa na mwendazake kwa muda mrefu.

Wanasiasa wengine hopeless kabisa! Sijui siasa walijifunziaga wapi. Yaani badala usifu kiongozi aliyeko madarakani unakalia kugombana na watu kutetea kiongozi ambaye ni Hayati!
 
Siasa ni mchezo wa ovyo siasa bila kuwa mnafk na kujishobokesha mambo hayaend siasa bila kuwa muongo hufanikiwi wanasiasa nawaona km madalali maneno mengi action zero
 
Back
Top Bottom