Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Luhaga Mpina anazingumza na Waandishi wa Habari kuhusu kinachoendelea kati yake na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuhusu hoja ya sukari ambayo ilianzia Bungeni.
======
Mpina asema wakati wa Mjadala wa kupisha makadirio ya mapato na matumizi aliagizwa na Spika wa Bunge kupeleka ushahidi wa kuwa Bashe amelidanganya Bunge. Mpina anasema alipewa siku muda hadi siku ya leo ya tar, 14/06/2024 na amedai tayari kashapeleka Ushahidi na vielelezo ambapo kwa kifupi anaeleza kuwa~~~~
Anasema Waziri wa kilmo Bashe wakati akichangia hoja ya Waziri wa Fedha alisema uongo mara 18, kama ilivyoanishwa kwenye ushahidi na vilelezo alivyokabidhi ofisi ya Spika, anadai, Maelezo ya Waziri mwaka jana 2023/2024 kwamba nchi hii mwaka jana kulikuwa na gape sugar ya tani 60000, walimpa Kagera Sugar, walimpa Bagamoyo, walimpa Mtibwa na Walimpa TBC na hakuna aliyeingiza hata kilo moja huo ni uongo.
Uongo wa Waziri uko katika maeneo yafuatayo, Gape sugar iliyoingizwa nchini ilikuwa ni tani 30000 na si tani 60000 kama Waziri alivyoliambia bunge.
Viwanda vya uzalisha vya sukari nchini hawakuleta hata tani moja pamoja na kuwapa kibali katika mwaka huo 2022/2023 kama alivyosema Bashe, Mpina amedai wazalishaji nchini pamoja na wafanya biashara waliingiza tani 6801 na hivyo si kweli kwamba hakuna hata tani moja iliyoingizwa nchini, Anadai ripoti ya CAG imeeleza kuwa tani hizo ziliingizwa nchini, hivyo waziri Bashe alilidanganya bunge.
Mpina anadai wenye viwanda walipewa vibali vya kuingiza Tani 2500 kila mmoja ambapo ni sawa na tani 12,500 ambapo vibali vyake vilitoka 3/ 5/2023 na kuishia 30/6/2023, vilikuwa vibali vya mezi mmoja tu na kitu, hivyo badala ya kuwalaumu waagiza wa sukari na wazalishaji wa sukari wa ndani kutoleta hata tani moja wakati vibali vyao vilikuwa vya muda wa mwezi mmoja tu. na Juni huwa wanaanza uzalishaji wasingeweza kwa kuwa vibali vilicheleweshwa na hivyo kuema hawakuingiza sukari ni uongo hata tani moja ni uongo.
Anadai Waziri Bashe alisema kuwa wameenda kubadili kanuni za National Food Reserve Agency kuruhusu NFRA kuwa na mandate ya kuagiza sukari hayo maelezo ni ya uongo hadi sasa hakuna GN yoyote ya Serikali inayoonesha kutungwa kwa kanuni mpya kuruhusu shirika hilo kuagiza na kusambaza na kuuza sukari hapa nchini.
Mpina anadai Waziri analalamika waliwapatia waagizaji walete nchini tani 50000, na hawakuleta hata tani moja ya sukari kufikia Mwezi Februari, kwa mwaka 2023/2024, tuna viwanda 5 na kila kimoja kilipewa kibali cha tani 10,000 kuingiza sukari tani 50000. Si sahihi kulaumu kutokuingiza sukari kufikia mwezi Feb. wakati Waziri anajua Vibali vilitolewa na bodi ya sukari tar 4 hadi tar 8 Januari 2024, hivyo isingewezekana ndani ya wiki 2 kuwa wameingiza sukari kwani inahitaji siku 60 hadi 90 na hivyo isingewezekana ndani ya mwezi 1.
Hata hivyo hadi kufikia tarehe 31 Mei 2024 jumla ya tani 49,884 zimeshaingizwa nchini na wazalishaji sukari kutokana na vibali vya kuingiza tani 50,000 walivyopewa mwezi Januari 2024 ambapo sukari hiyo imesambazwa sehemu mbalimbali nchini.
----
Hayo ni sehemu ya hoja aliyozungumza Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina alipokutana na wanahabari jijini Dodoma leo, Ijumaa Juni 14.2024 ambapo ametumia jukwaa hilo kufafanua hoja alizodai kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amelidanganya Bunge wakati akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha Bungeni hivi karibuni.
Pia soma:

- FULL TEXT: Maelezo ya Ushahidi Wa Luhaga Mpina Kwa Spika Wa Bunge Dkt Tulia Ackson juu ya Waziri Hussein Bashe Kusema Uongo Bungeni kuhusu Sukari
- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
- Luhaga Mpina: Waziri Bashe na Mwigulu walitengeneza uhaba wa sukari nchini, zilikuwa njama za kuiba mapato ya nchi