Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE LUHAGA MPINA ASHAURI MWENGE WA UHURU UPITIE MIRADI YOTE
Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Joelson Mpina ameishauri Serikali kurekebisha muundo wa mbio za Mwenge wa uhuru badala ya kupita kwenye Miradi ya Halmashauri pekee ipite na kwenye Miradi Yote
Akizungumza na waandishi wa habari Babati mkoani Manyara Mpina amesema kuwa Miradi ya SGR, TANESCO na Miradi mingine ijumuishwe katika mbio za Mwenge wa uhuru ili kama kuna changamoto yoyote hatua ichukuliwe dhidi ya mhusika
Pia amesema kuwa Kila mwaka mwenge wa uhuru unabaini ubadilifu wa fedha,wizi na Nyaraka lakini Serikali haichukui hatua dhidi ya wahusika hivyo ameishauri Serikali Kila mwaka kuwe na taarifa ya maelekezo yalizochukua dhidi ya wahusika wanaokwamisha Miradi ya Serikali
Mpina amemalizia kusema kuwa mwenge wa uhuru uwekewe Utaratibu mzuri wa kufika Hadi vijijini maana Kila mwaka mwenge unazunguka katikati ya Halmashauri hiyo itasaidia kupeleka huduma za kutosha vijijini ambapo ndipo Kuna changamoto kubwa sana ya miundombinu