Luhaga Mpina asema CCM haiwezi kumfukuza jembe kama yeye.
Asisitiza kuendelea kudeal na mafisadi, hataangalia sura ya mtu, Rangi, Wala kujuana na wakubwa, asisitiza kusimamia misingi ya uanzishwaji wa CCM na aliapa kulinda katiba ya CCM na ya Nchi, asema msisitizo wa Muongozo wa CCM Uko wazi na Uko Uk wa Mwanzo wa katiba.
Mpina alisema alipiga spana kwa Mawaziri wanaokiuka misingi kwa kupitisha mikataba ya Hovyo kuwapa mabosi zao, la Sukari bado bichiii, aliyeunda kampuni uchwara kujipatia vibali vya Sukari kwa kampuni za simu, stationery nk zisizo na mtaji Hata wa Milioni 30 kuwekwa wazi.
Haiwezekani Sukari shehena iwe Tani kwa Tani kwa mabilioni kwa mabilioni leo Apewe mtu Mwenye mtaji wa Milioni 10 aagize Lazima ukiona kifaranga Cha Kuku kinatamba jua mama yake Yuko pembeni tu, so kutamba kwa Waziri wa kilimo Hussein Bashe Basi Rostam Aziz yupo karibu.
Amalizia kwa kusema wale waliokuwa wanachezea Umeme wetu na mawasiliano wako pembeni hivyo bado mmoja.