Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Wakuu hamjamboni nyote...
Nadhani wote mnamfatilia Luhaga Mpina Mbunge wa Kisesa na Kada Kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi, Namna anavyozungumzia uongozi uliopo wa CCM na serikali kwa mtazamo hasi. Kwa namna na minajili hiyo na kwa mfumo wa CCM ni wazi hataweza kukubalika kuendelea na uanachama. Yupo kinyume kabisa na mila na tamaduni za Chama.
Sasa Huku kwetu tumepata taarifa kutoka kwa chanzo cha karibu na Uongozi wa juu wa Chadema kwamba ile nafasi moja aliyotangaza mwenyekiti wa CDM ndugu Tundu Antipas Lissu ya kuiacha wazi kwenye kikao kikubwa kabisa cha maamuzi ndani ya chama (Kamati Kuu) ili kusubiri mu/waenguliwa toka CCM, basi ni ya LUHAGA MPINA. Huyu mtu ameombwa na kukaribishwa CDM kutokana na uthubutu na umahiri wake katika kukosoa na kutoa mitazamo yake juu ya uongozi wa serikali.
Kwa maoni yangu inawezekana hii ikawa ni turufu au mtego kwa CDM katika kuelekea Uchaguzi mkuu. Wawe makini tu.
Mwisho wa siku tunataka siasa safi na uongozi bora kutuletea maendeleo wananchi na kupinga kila aina ya ufisadi na ubadhirifu wa mali za uma.