BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mbunge wa Jimbo la Kisesa lililopo mkoani Simiyu Luhaga Mpina akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mpina (Mpina Stadium) Jumapili Agosti 11, 2024.
Mpina amesema "Baada ya mimi kusimamishwa vikao 15 kwa makosa ya kusingiziwa na kuonewa na pia kutoridhika na uamuzi huo, nikaamua kwenda mahakamani, nitaendelea kusimama imara kwenye kesi niliyoifungua dhidi ya Spika wa Bunge, lakini pia kesi ya pili nimemfungulia kesi Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na kampuni za ITEL, Zenji Industries, Mohamed Enterprises kwa makosa ya kuagiza sukari nje ya nchi zaidi ya kiwango kinachohitajika na kusababisha madhara makubwa kwa Watanzania,
Kutumia makampuni yasiyoruhusiwa kisheria kuagiza sukari, kuagiza sukari ambayo haina viwango, kutoa misamaha ya kodi kinyume cha sheria na yenye upendeleo, inayotupotezea mapato. Tunakwenda kupoteza zaidi ya trilioni moja na tumeshapoteza zaidi ya Shilingi trilioni 1.54. Watuhumiwa wote hawa watakuwa kwenye kesi na tarehe 28 Agosti, 2024 kesi hii itaanza"- Mpina.
Mimi (Luhaga Mpina) ni mtaalamu wa fedha tena siyo wa kubahatisha, ninazijua namba na sina sababu ya kumsingizia mtu, ndiyo maana mambo yote ninayosema, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akija kukagua anasema vilevile kama ambavyo mimi nasema. Kwa hiyo sibahatishi katika kutengeneza namba, sibahatishi kwenye uhasibu wangu na pia sibahatishi katika Financial Analysis (uchambuzi wa masuala ya kifedha), nilichokisema nina uhakika nacho, ndiyo maana nimewapeleka (Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengineo) mahakamani kwa kuwa bungeni sikusikilizwa. Niliwasilisha bungeni tuhuma za watu ambao walilisababishia taifa hasara ya Shilingi trilioni 1.54 badala yake nikafukuzwa bungeni, badala ya ninaowatuhumu kuchunguzwa na makosa yao yakafahamika ili kama mimi Mpina ni muongo basi uongo wangu ungejulikana. Kwanini niondolewe bungeni?”- Mpina.