Luhaga Mpina: Wafanyabiashara kudaiwa kodi kubwa kuliko biashara zao inatoka na usimamizi mbaya wa ukusanyaji wa kodi

Luhaga Mpina: Wafanyabiashara kudaiwa kodi kubwa kuliko biashara zao inatoka na usimamizi mbaya wa ukusanyaji wa kodi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Luhaga Mpina anaunguruma muda huu Sakasaka Jimbo kwake Kisesa

Updates......
Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina amendelea kufanya ziara katika jimbo lake hilo kusikiliza kero za wananchi leo kata ya Sakasaka.

Mbunge Mpina amewataka wananchi wa Jimbo la Kisesa kuchukua hatua ili kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa kuwataka kula chakula safi kutumia maji masafi. Ambapo ugonjwa huo umeibuka kwa wakazi wa Kata ya Sakasaka.

Mpina amesema kutokana na chagamoto ya kukosekana kwa dripu kwenye baadhi ya Zahanati ya Sakasaka katika jimbo hilo amewaahidi Wananchi wake kuleta dripu 500 kufika kesho ili ziweze kuwasidia wagonjwa ambao watahitajika kupewa dripu.

Aidha Mbunge Mpina amesema wametenga bajeti ya Milioni 207 kwaajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Sakasaka kwenda Bwiwandulu kwenda Mwatambuka hadi Matale na hadi sasa Mkandarasi ameshapatika na kuanza kasi mwezi wa tisa 2024.

Amewataka wananchi wa Sakasaka kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika 27 November, 2024.

"Chama Cha Mapinduzi hakuna mahala kiliporuhusu zuluma, Rushwa na Ufisadi na mambo mengine" amesema Luhaga Mpina.

Aidha amewataka Wanasiasa kuacha kufanya siasa za kishamba na kufanya Siasa za maendeleo za kujenga Wananchi.

Wafanyabiashara wetu kudaiwa kodi kubwa kuliko biashara zao Mwananchi anabiashara ya Milioni 1 anaombwa kulipa kodi ya milioni 1 na laki 5 lakini hii yote inatoka na usimamizi mpya wa ukusanyaji wa kodi nchini amesema Mbunge Mpina.

Mpina ameendelea kusema lazima ulipaji wa kodi nchini uwe wa usawa watu walipe kodi kwa usawa mtu alipe kodi kwa mujibu wa sheria lakini kwa kiwango kinacho ruhusuwa na kiwango kinacholingana na biashara yake.


View: https://www.youtube.com/watch?v=4ToXKwl6yS0
 
Ashirikiane na hao wakazi wa sakasaka kusafisha maeneo na kuhakikisha Kila kaya inakuwa na choo Bora zikiwepo taasisi kama shule
Drip ni suluhisho la mda mfupi sana
 
Back
Top Bottom