Luhaga Mpina, Waziri kavunja Sheria hatangazi tenda kuagiza Sukari nje; Waziri kasema ni kweli tenda hazitangawi. Eti leta ushahidi?

Luhaga Mpina, Waziri kavunja Sheria hatangazi tenda kuagiza Sukari nje; Waziri kasema ni kweli tenda hazitangawi. Eti leta ushahidi?

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
Kuna mambo yanaendelea mpaka unashikwa na hasira na kutamani kupiga ukuta ngumi. Sasa Mh mpina kasema waziri kavunja sheria, Tenda zote za Kuagiza sukari nje hazitangazwi kinyume na sheria na taratibu. Wakati akijibu Mh Waziri wa Kilimo akasema ni kweli tenda hazitangazwi. Hivi kwa mlinganisho wa kimatiki unahitaji ushahidi hapa?

Je, tukisema huu ni upigaji wa kimkakati utakataa, Waziri anaijua sheria, anajua taratibu, hajasahau kwani amezungukwa na wakurugenzi na kamati mbalimbali kumkumbusha. Kwa hiyo sula la alipitiwa, amesahau, it was an overlook hakuna, sikubali na sitakuja kuhafiki hiyo sababu.

Kwa usahaulifu wa kimkakati kama huo unatufanya tuwaze tofauti, tuwaze lazima kuna kisahaulishi ndio maana yeye waziri na team yake nzima wakasahau, wakaoverlook very important mandatory procedure, basi wamesahau taratibu zao je wameshahau na procurement act ya tendering of major national procurement?

Je, tukisema na kufikiri hii inampa mamlaka Mh na team yake kuchangua mtu wao, anaweza kuwa Ngosha, Masawe, Mboni, Kimji, Abdalah, Patel.Kumbuka hii ni multinational and multibillion tender na it is a repeated tender , just imagine a guarantee ya tender ya 150 Tsh billions , je 10% yake ni shillingi ngapi? hapa unaongelea mabiilioni zaidi ya kumi na kizuri zaidi it is a repeated tender. How much are they illegally earning per two, three, four tenders?

Ifike mahali tukubali mapungufu ili maisha yaendelee na huo ndio uhungwana. Tunapomuattack mwakilishi wa wananchi kwa kusema ukweli, inamaanisha tunawapa taarifa, onyo, tahadhali na wabunge machachali wengine wote wasithubutu kusema ukweli. Je, hilo litakuwa ni Bunge la wananchi au ni bunge la wala nchi.

Pia Soma Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
 
Habari yako ina mkanganyiko.... unaweza kuweka ad verbum majibu aliyotoa Waziri ?
 
Habari yako ina mkanganyiko.... unaweza kuweka ad verbum majibu aliyotoa Waziri ?
Unaweza kuweka hiyo ad verbum wewe, mimi nimeweka sehemu ya kilichoongelewa . Suala la kujiuliza je kiliongelewa au hakikuongelewa? na suala la kuleta ushahidi limeongelewa au halikuongelewa. Hakuna sheria ya uhandishi (writting style) ndani ya platform yetu pendwa ya Jamii forum. Kila mtu ana jinsi ya kuandika na kumake a case jinsi itakavomplease namna ya kuwakilisha hoja.
 
wewe ndio umeleta habari wala sijakulazimisha..., mimi nimekuuliza kama unaweza kuweka ad verbum alichosema sababu sikusikia sasa kama huwezi na lenyewe ni poa tu...

Kuhusu kama yaliyongelea au hayakuongelewa mimi sijui wewe unayejua ndio umeleta habari kama kila mtu angejua basi kungekuwa hakuna sababu ya wewe kuleta habari
 
Kwa sasa kuna watu watatu ndo naona hao ni binadam na wanautendea haki uongozi Mpina Makomda na jerry slaaa hawa watu Mungu awatunze sana hata kama wanaubaya ila wanajitahidi sana kutenda haki...
 
wewe ndio umeleta habari wala sijakulazimisha..., mimi nimekuuliza kama unaweza kuweka ad verbum alichosema sababu sikusikia sasa kama huwezi na lenyewe ni poa tu...

Kuhusu kama yaliyongelea au hayakuongelewa mimi sijui wewe unayejua ndio umeleta habari kama kila mtu angejua basi kungekuwa hakuna sababu ya wewe kuleta habari
Sasa unauliza kitu ambacho hujui kama kiliongelewa.Do sawa bwana
 
Mtu ye yote akijisahaulisha sheria yo yote ya nchi kwa manufaa yake ni mhujumu uchumi na anatakiwa achukuliwe hatua kali za kisheria!
 
Back
Top Bottom