Luhanga Mpina aibua mambo ya kutisha huduma za kuongeza makalio, atoa ufafanuzi mzito

Serikali inajifitini sana kupitia viongozi wake waandamizi
 
Hi nchi hii! Watu wanaishi kwa buku jero kwa siku, lakini serikali inaona jambo LA maana ni kuleta huduma ya kuongeza makalio na matiti!
Ni ama serikali imejaa machizi!au wameamua kuchezea saikolojia za wananchi ili kutupumbaza, kutukera, kufanya tuache kufatilia Mambo ya msingi tuongelee huu upuluzi
 
Mpina ana hoja kubwa sana na bahati mbaya sana itadharauliwa na kutupwa kapuni.

Madhara na matokeo ya hoja za Mpina tutayaona sio miaka mingi sana ijayo, ambapo vijana wakike kwa wakiume akili zao zitakapokua zinaongozwa na matako.
 
Haya maswala ya kutengeneza shape ni maswala ya mtu mmoja mmoja (binafsi) hayana mantiki na wala sisi kama wananchi wa kawaida hatuoni kama yana mantiki.

Serikali ipambane wananchi wapate huduma muhimu. Yani watu wanakosa hadi sukari tu ya matumizi ya kila siku kisha wao badala ya kuangalia wanamalizaje tatizo wako busy wanagombania kukuza makalio?? Kwakweli ni aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…