Luis Figo ajitosa kuwania Urais wa FIFA

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Luis Figo ametoa taarifa za kushitusha baada ya kutangaza kuwania Uraisi wa FIFA.


Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Sporting Lisbon, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan mwenye miaka 42 anaungana na mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola katika kuwania nafasi ya kumng'oa madarakani bosi wa sasa Sepp Blatter katika chombo hicho kikubwa cha soka duniani.


Wengine wanaowania kiti hicho mpaka sasa ni Mfalme Ali wa Jordan, Michael van Praag na Jerome Champagne.


Blatter amekuwa kiongozi wa shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na akitaka kuendelea kuwania tena uongozi katika awamu ya tano.


Wagombea wote wanaowania kiti hicho wanatakiwa kujiandikisha kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Alhamisi.


Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati ya uchaguzi Dominico Scala, wagombea wote wanatakiwa kupitishwa na kamati ya FIFA ya kuzuia rushwa michezoni.


Mwaka 2000 Figo aliweka rekodi ya uhamisho wa kiasi cha pauni milioni 37 baada ya kuhama Barcelona kwenda Real Madrid pia
Figo ameichezea timu ya taifa ya Ureno mara 127 na aliwahi kutwaa ubigwa wa Ulaya akiwa na Real Madrid 2002.


Pia aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2000 na mwaka 2001 akatwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Fifa.


Chanzo:Clouds FM
 
Anayeweza kumuondoa Blatter hapo ni Platini peke yake..Wengine wote hawamuezi huyu babu..Kwanza Africa nzima isha pledge kumpa kura..
 
ila huyo mzee kakaa kwenye position hiyo kwa muda mrefu awaachie na wengine sasa...au na yeye kakomaa hataki kung'oka kama Mugabe!!!
 
Huyu mzee amekaa muda mrefu sana ni vizuri sasa awapishe wengine, ni uamuzi mzuri tu kwa Figo namtakia kila la heri.
 
Platini ndo atamtoa ila amekataa kugombania pamoja na huyu Babu. Natumai akistaafu atajiunga kwenye kugombea uraisi wa FIFA
 
Hana uwezo huo, kama Bin Hammam alimshindwa Blatter seuze Figo?

Ishu hapo ni fungu na sio ushawishi wa mhusika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…