Luis Miqsonne avunja mkataba na Al Ahly

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001


Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka Misri, Club ya Al Ahly ya Misri imevunja Mkataba na Mchezaji wa Kimataifa wa Msumbiji Luis Jose Miquissone kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Miquissone alijiunga na Al Ahly ya Misri akitokea Simba SC ya Tanzania 2021 ila amekosa nafasi ya kucheza toka aondoke Kocha Pitso Mosimane na sasa amevunja mkataba ili aende sehemu atakayopata nafasi ya kucheza.

Asilimia 90 Luis Jose Miquissone anarudi Simba SC inaeleza ameshakubaliana maslahi binafsi na Uongozi.
 
Kweli tusimdharau Hersi kwasababu ya jeans yake imechanika, bali tuiangalie akili yake.

 
Mchezaji wa Kimataifa wa Msumbiji na timu ya AL Ahly Luis Miquissone amefikia tamati na timu yake hiyo ya Misri hivyo muda wowote atakuwa mitaa fulani ya Dar es Salaam kuanza maisha mapya ya kisoka.

 
Nini kilomkalisha mwaka mzima bila kucheza huko Misri?
Hili swali kamuulize Percy Tau naamini anayo majibu yeye kuchezea Brighton Hove Albion niamini anayo majibu mujarab!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…