Lulu ampora bwana Hamisa Mobeto

Lulu ampora bwana Hamisa Mobeto

mchepuko

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,192
Reaction score
1,415

Mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto.

MAPENZI ya mjini utata mtupu! Ni kauli inayostahili kutumika baada ya mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto kumwaga chozi akidai kuporwa bwanake aliyekuwa akimpa jeuri mjini (jina tunalo) huku zigo la lawama likimwangukia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Lulu.

CHANZO KINASEMAJE?

Habari kutoka kwa chanzo makini zilieleza kwamba, kwa sasa kuna bifu jipya linalotokota mjini likihusisha sakata la Lulu kumpiku Mobeto kwa bwanake aliyekuwa akimgharamia kiasi cha kuwa mwanaume pekee aliyemwamini hadi kufikia hatua ya kumzalia mtoto.


Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Lulu.


Ilidaiwa kwamba, jambo hilo Lulu hakulithamini na kuamua kumpiku huku akimuacha akiishia kulalama kila kukicha.

Najua hamuujui mchongo huu. Sasa ngoja niwapashe habari kwa kina. Nimeamini Lulu kweli ni jasiri, maana kwa alichomfanyia Mobeto Mungu ndiye anajua.

PEDESHEE MPYA WA LULU
Huwezi kuamini yule bwana wa Mobeto Lulu kaamua kujiweka kwake, inaweza kuwa ngumu watu kukubali lakini ndiyo ukweli wenyewe.

Unaambiwa mtiti wa Mobeto na Lulu ulianza kama mwezi mmoja uliopita. Walianza kwa kuandikana kwa mafumbo kama waimba taarab kwenye mitandao ya kijamii.

MAFUMBO INSTAGRAM
Nimekutana na rafiki wa Mobeto ndiye kanipa mkanda wote kuwa Lulu kampiku Mobeto kwa bwana?ke ndiyo maana mafumbo hayaishi Instagram.

MOBETO HATAKI KUMSIKIA LULU

Kwa sasa Mobeto hataki kusikia habari za Lulu na ukimuuliza anasema Mungu atamlipia kwani anamshukuru kumtoa huko kwani alipo sasa ana amani tele,? kilidai chanzo hicho.

MOBETO AFUNGUKA MAZITO
Kwa upande wake, Mobeto alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kuwa kwa sasa ana mambo yake mengine hivyo habari za Lulu ingekuwa vizuri akaulizwa yeye na huyo bwanake.

Mobeto alisema kuwa kwa sasa anachoweza kuzungumzia ni juu ya maisha ya mama yake mzazi na mtoto wake kwani hao ndiyo faraja pekee iliyobaki kwake.

Alisema kuwa, hapendi kuzungumzia mambo yaliyopita kwani kila jaribu lina mlango wake wa kutokea hivyo yawezekana yote Mungu aliyapanga akiwa na sababu za msingi.

?Mambo hayo mimi sitaki hata kuyazungumzia kwa sasa, nafikiri ingekuwa vyema ukamuuliza Lulu na ?.(anamtaja huyo mwanaume) kwani wao ndiyo wanaweza kukupa ukweli na kukusimulia kiunagaubaga.

MOBETO AMWACHIA MUNGU
Katika maisha yangu, kwa sasa namwangalia mtoto na mama yangu, hao wakikosa furaha hata mimi siwezi kuwa na amani kwenye maisha yangu, kwani mambo mengine yakishapita hakuna sababu ya kuyaendeleza zaidi namshukuru Mungu.

Kwa sasa nina michongo yangu mipya na siko tayari tena kuzungumzia habari nje ya familia yangu.

Ninachoweza kukuambia ni kwamba maisha yana kila staili ya kuishi hivyo sifikirii tena kuingia kwenye mitandao ya kijamii kuzungumzia habari za mtu kwani hata hao wanaonizungumzia sina muda wa kuanza kusoma comments (maoni) zao wala kuwajibu.

Kwa kifupi sijawahi hata kuona mambo yanayozungumzwa kuhusu mimi kwenye mitandao maana huwa sisomi tena kwani kila mtu ana namna ya maisha aliyochagua.

Hata huyo Lulu na timu zake mimi sina muda wa kusoma mambo yao kwani Mungu ndiye tegemeo langu, alisema Mobeto.


LULU ARUKA MITA MIA

Alipotafutwa Lulu na kupewa taarifa za uporaji wa bwana wa mtu, aliruka mita mia moja kwa kusema kuwa habari hiyo ni mpya kwake na hajawahi kusikia lolote ila ndiyo anaambiwa kwa sasa hivyo kama kuna mtu ana picha zake na huyo bwana wa Mobeto, basi ndiyo anapata taarifa.

Madai haya kwangu ni mapya na siyajui ndiyo mnaniambia kwa mara ya kwanza, sioni sababu ya kulizungumzia, alisema Lulu.
 
Halafu unaweza kuta huyo jamaa mwenyewe mume wa mtu au kashazaa na visichana kibao hapa twn
Kweli wanaume kwa sasa ni viumbe hadim
 
Duh ndo yule dj majay leo kawa pedeshee..bongo tambarare
 
Duh yule jamaa ameachana na hamisa??? Poor her ndo maana sahivi anajichanganya zake viwanja mara dubai mara wapi kumbe anatoa stress.... Pole zake, ila lulu nae kavalishwa Pete ina maana majizo ndo kamvalisha eeh makubwa haya
 
PROMO...haya mabeto yupo single tena, mwingine akarithi mzigo sema ajiandae kua baba wa kufikia.
 
Lulu ana laana ya dunia. Asubir kifo sasa hiv maana jela haikumfunza
 
Lulu naona anataka kumrestisha in peace huyo majizo. Hamisa naye kilichomfanya amzalie mtoto mapema mini? Majizo kazaa na wanawake ka wawili. Pole yako hamisa
 
Vijana wakibongo ukitaka kutoka nikufanya kazi kwa bidii weledi na kusave. Vingine hivyo nikubahatisha tu!
 
Huyo dj majizo kwanza sio mzima. Wasanii huwa hawapimi, wao wanaanzisha uhusiano tu. Cjui wenzetu ni immune kwa Hechiaivii
 
Huuo lulu ni star wa filamu gani bongo japa? Mana sioni filamu zake ila nasikia ni star wa filamu bongo.
 
Majizo mwenyewe sura nzito labda kama faragha yuko vzuri mmmh lakin sura hapana
 
Kuna watu wanaongea kama wanamjua Francis vizuri. Daaah haya kila mtu la lwake.
 
Back
Top Bottom