Lulu atatoka

Lulu atatoka

vipik2

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
2,845
Reaction score
2,258
Jaji aliyepangiwa ...Kusini na Mashariki zote zinalingana,





Dhamana: Mawakili wa "Lulu" wawasilisha maombi; Kusikilizwa Ijumaa, Januari 25

21/01/2013
0 Comments


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Ijumaa, Januari 25 mwaka huu, itasikiliza ombi la kupatiwa dhamana msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael Lulu aliyepo katika gereza la Segerea akikabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia Na. 125/2012 msainii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Ombi hilo la dhamana ambalo tayari limeishapangiwa Jaji Zainabu Mruke kuanza kulisikiliza ombi hilo wakati bado kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa, limewasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa Lulu, na wake Peter Kibatala, Kennedu Fungamtama na Fulgence Massawe.

Kwa mujibu wa hati ya ombi hilo la dhamana, mawakili wa Lulu wameonyesha kuwa ombi lao wameliwasilisha chini ya kifungu cha 148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .
Lulu ni mtu maarufu nchini, anaiomba mahakama hii impatie dhamana na yupo tayari kutimiza masharti ya dhamana yatakayo tajwa na mahakama hii, na anaahidi kuyatimiza masharti hayo wakati akisubiri kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia itakapopangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa katika mahakama yako tukufu.
Alidai Wakili Kibatala katika hati hiyo.

Desemba 21 mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi tisa.

Hapiness Katabazi

Source: Previous Posts - wavuti.com
 
Mbunge Komba atakuwa anamsubilia kwa hamu litamgonga kwa hasira ile mbaya
 
Kama Lulu aliua bila kukusudia, alimuuaje sasa marehemu Kanumba? Maana hakuna eyewitness yeyote aliyekuwepo chumbani. Walikuwamo wao wawili tu.

So how exactly did she kill him? The prosecution has an uphill battle proving that charge. I just don't see how they win this case.
 
SECTION NUMBEr 18B (1),(2),(3) OF TANZANIA PENAL CODE IMEELEZA WAZI KWAMBA ANY PERSON WHO CAUSES THE DEATH OF ANOTHER AS THE RESULT OF EXCESSIVE FORCE USED IN DEFENCE ,SHALL BE GUILTY OF MANSLAUGHTER , HUYY LULU ALIKUWA ANTUMIA KUJIKINGA LAKINI FORCE ALIYOITUMIA HAIKUWA ILIZIDI LAKINI CHA KUSHUKURU NI KWAMBA KASHABADILISHIWA KESI
 
According to me naona she is not to be convicted for muder kwa kua hapakua na mensrea ni Act iliochotokea kwa mda mfupi sidhani kama kulikua na intetion yoyote au mnaonaje wataalamu?
 
Back
Top Bottom