Lulu Diva Ashindwa Kuzizuia Hisia Zake Kwa Chid Benz

Rugaikamu

Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
37
Reaction score
20
HUKU wasanii mbalimbali wakimtaka rapa mkali Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, chipukizi anayefanya poa kwenye gemu la muziki, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ naye amemlilia, akisema kitendo chake cha kuendelea na ‘unga’ kinamuumiza.

Akipiga stori na Risasi Vibes, alisema jambo hilo linamuumiza kwa vile tangu akisoma alikuwa akifuatilia muziki wake, hivyo ni vyema kama angeachana na mambo hayo yasiyo na faida ili arejeshe heshima yake katika muziki.

“Namshauri Chid aachane na hayo mambo mengine, atulize akili yake kwenye muziki, naamini atafanya vizuri na kujiingizia kipato kizuri maana muziki wa sasa unalipa, ili ufanikiwe kwenye hii fani lazima utulize akili uipende na uipe heshima, akizingatia haya atarudi kwenye ubora wake,” alisema
 
Huyu dada uwa anapendeza asipojipiga na make up mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…