Lulu (Elizabeth Michael) kuachiwa kwa dhamana

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,878
Reaction score
5,432


Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mahakama kuu ya Tanzania imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.

Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.

Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza.

SOURCE: ITV


UPDATES:

- Sasa ndio wanakagua documents za wadhamini mahakamani...
- Kuna mambo hayajakamilika hivyo anarudi jela, hadi kesho...

FINAL UPDATE (03:00 PM, 28, Jan, 2013)
Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho kwakuwa Msajili wa Mahakama Kuu hakuwepo na hii ilikuwa ni kesi ya 'Kuua bila kukusudia'.

Kesho wadhamini watawasilisha nyaraka zao mbele ya msajili ndipo anaweza kuachiwa...

Tutawafahamisha kitachojiri mahakamani kesho


 
Pole zake lulu,, mwache arudi nyumbani apumzike maana mwaka 2012 hatausahau maishani mwake...

Wenye uelewa wa mambo ya dhamana mnisaidie ili swali " hivi hiyo hela aliyotolewa dhamana itarudishwa kama akishinda kesi au ndo mali ya mahakama?
 
Pole zake lulu,, mwache arudi nyumbani apumzike maana mwaka 2012 hatausahau maishani mwake...

Wenye uelewa wa mambo ya dhamana mnisaidie ili swali " hivi hiyo hela aliyotolewa dhamana itarudishwa kama akishinda kesi au ndo mali ya mahakama?

Haiwezi kuwa mali ya mahakama ashinde asishinde anarudishiwa.Hiyo inakuwa mahakamani kama endapo akitoroka ndiyo inakuwa sehemu ya malipo ya mlalamikaji/mahakama.
 
It will take her only three months to forget, and she will go back to square one.
 
Inabidi nimtafute lulu wangu leo baada ya kuachiwa tukapate chakula pamoja..najua atakua na hamuuuuu si ujua siku nyingi..ila nasikia anamimba???
 
Atakuwa na hamu mpaka inamzidia hamu,embu mtafte fasta kabla hajaanza mambo yetu yalee.
 
Kwa taarifa zilizotangwaza n itv sio muda mrefu mtuhumiwa wa mauji ya stiven kanumba ameachiwa kwa dhamana naomba mlio karibu mfuatilie hiihabari
 
masharti ni kuwa anatakiwa awe na wadhani wawili wanaofanya kazi serikali walio na kiasi cha 20 millions tsh. pia awe asitoke nje ya dar bila ruhusa na document zake zote kama passport ya kusafiria anatakiwa aziwasilishe mahakani
 
Sasa akatulie huko nyumbani, sio azekurukaruka na magazeti, itamualibia katika kesi yake
 
Akina Ruge na Shigongo washapata dili.

Watatulipisha viingilio kwenda kumuona Dar live na ziara za mikoani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…