Lulu Michael Aipa Shikamoo Pombe...

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
Star wa Bongo Movies Lulu Michael, ambaye pia anakisiwa kuwa miongoni mwa wanawake warembo afrika nzima katika tasnia ya filamu, ameipa mkono waburiani utumizi wa vileo.

Kulingana na staa huyu mwenye urembo wa kuvutia amesema kuwa pombe ni chanzo kikuu cha maovu katika maisha ya binadamu.

Lulu amekiri kuwa tangu atoke gerezani ameamua kuachana na uraibu wa kunywa pombe na yuko radhi kuitwa mshamba kwa jambo hilo.

"Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo kichocheo cha kila baya hapa duniani,watakaoniona mshamba kwa kubadilika kwangu wanione hivyohivyo," alisema mrembo huyu.

Msanii huyu ambaye yuko katika kipindi cha Nyumba alikuwa mlevi wa kupindukia na kuna wakati mmoja alishawahi kuzidiwa na video katika Maisha Club jijini Dar.

Chanzo: bkuHABARI
 
Adolescent ni hatua ambayo kila mtu anapitia...alikuwa mlevi lini wakati alikuwa bado mtoto.
 
mwambie huyo anakurupuka tu na sifa za ajabu ajabu

kila kitu kina sababu yake,bila kwenda gerezani na kujifunza maisha yapoje asingeacha kiurahisi,kwahiyo gereza limemfunza. Kama anayosema ni ya dhati nampa big up. Pombe bila mpango inakushusha hadhi.
 
mtoto ndo kwanza sijui ana miaka 18 sijui 19?

mwacheni tu akue.. tuna mengi sana ya kuona na kusikia!

nguruwe pita.. leo sina mkuki!
 
wakaache ka lulu kadogo
no one is perfect
 
Njia ya kutafuta bwana wa kueleweka.wengi wanakaogopa kwa issue ya mauaji.
 
Kweli we learn from mistake
kwa kweli kafanya jambo la maana lakin will she keep it up
Bila kunywa pombeee
 
Kusema Lulu ni miongoni mwa wazuri Africa, sijui Top Ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…