LULU Michael na madai ya kulipwa mil. 15

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Sidhani kama kuna producer apa bongo mwenye kifafa cha akili, ambaye ataweza kumlipa LULU mil 15 kwa movie moja tu. Achilia mbali uigizaji mbovu Wa Lulu Michael, hakuna movie yeyote aliyowahi kuigiza LULU na kuweza kuvunja rekodi ya mauzo kuliko filamu nyingine yoyote hapa nchini na kuweza kuwashawishi ma producer kuweza kumtumia kwenye movie zao ata kwa dau la mil 5 tu.

Nina uhakika LULU anaweza kuongoza kwa mauzo ya magazeti ya udaku apa nchini, ila sio kwenye filamu za kibongo, huo ndio ukweli.

Siwezi kumlipa Shamsa ford (CHAUSIKU) laki Mbili na nusu kwenye movie ya CHAUSIKU then nikamlipe LULU mil 10 akaigize FOOLISH AGE, that is foolish.

Ni upuuzi kumlipa RIYAMA ALLY laki tatu kucheza filamu ya FUNGU LA KUKOSA nikamlipe LULU mil 6 kucheza movie ya FAMILY CURSE.

Ni laana kumlipa ODAMA (Jennifer kyaka) laki tatu kucheza filamu ya ODAMA ukamlipe LULU mil 8 kucheza movie ya FAMILY DISASTER.

Hakuna awezaye kumlipa NISHA (salma jabu) laki moja na nusu kucheza filamu ya ZENA NA BETINA ukamlipe LULU mil 20 kucheza movie ya HOUSEBOY.

Simaanishi kuwa LULU sio muigizaji mzuri ila kiwango chake kwenye tasnia ya filamu bado sana , she has a long way to go, asifananishe umaarufu Wa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii na kiwango cha uigizaji wake kwenye tasnia ya filamu.
 
Hahahaaa warumi umenichekesha sana. Inamaana hao bongo movie's hua wanalipwa laki laki au? Maana naona Lulu tu ndiye anayelipwa cha juu hapo.
 
Last edited by a moderator:
uchi ndo unamwingizia pesa na wala si movie. Sasa hvi anatoka na mtoto wa mzee wa kuteua wakuu wa wilaya, riz1
 
uchi ndo unamwingizia pesa na wala si movie. Sasa hvi anatoka na mtoto wa mzee wa kuteua wakuu wa wilaya, riz1

Kuna watu wana bahati... hawa waheshimiwa wanapatikana wapi nijisevia mmoja.

Binamu huyo Chausiku niliona ile movie yake maana ilibidi niitafute kwa jinsi watu walivuokua wanaisifia.... anavaa uhusika balaa.
 
Hahahaaa warumi umenichekesha sana. Inamaana hao bongo movie's hua wanalipwa laki laki au? Maana naona Lulu tu ndiye anayelipwa cha juu hapo.

Bongo movie wanalipwa kuanzia laki mbili ikizidi sana sita au nane ila kuna wengine wanajilipa mil 15 wenyewe ila sio kweli wanalipwaga Pesa ndefu kihivyo..ma producer ndo wanavijihela kidogo
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wana bahati... hawa waheshimiwa wanapatikana wapi nijisevia mmoja.

Binamu huyo Chausiku niliona ile movie yake maana ilibidi niitafute kwa jinsi watu walivuokua wanaisifia.... anavaa uhusika balaa.

Ebu sema na wewe hyo million kumi na tano ungempa lulu au yule chausiku? Kuna watu wanaigiza mpaka unakaa chini unajiuliza Mara mbili katoa wapi kipaji..lulu bado sana kufikia level za shamsa na riyama
 
Mkuu warumi kwanza asante kwa taarifa ya mapato ya huyu binti katika kazi zake mbalimbali. Lakini mkuu pamoja na kwamba mwishoni umejitahidi kuonesha kwamba humkandii lakini ulivyoandika ni kama una-underate kazi za lulu. Labda nikukumbushe kidogo lulu ni mwigizaji pekee kwenye tasnia ya bongo movie aliyeanza kazi hiyo akiwa na umri mdogo sana. Kipindi cha nyumba hii sanaa ilikuwa hailipi hivyi inawezekana kabisa muda wote huo alikuwa analipwa kiduchu. I think ni muda mwafaka kwa huyu mdada kufurahia matunda ya kazi yake. Tuoneshe uzalendo kwa kumtia moyo, sema mapungufu yake ni yapi ili ajirekebishe. Kati ya makosa makubwa tunayofanya wabongo ni kufuatilia maisha binafsi ya wasanii which is wrong. Let's b positive to our artists and provide constructive criticism. Ni mtizamo wangu.
 
Last edited by a moderator:

Mimi uwa nafuatilia sana kazi za apa nyumbani especially bongo movie, lulu bado hana kiwango hicho kusema alipwe million 15 labda magazeti ya shigongo yalimpe hyo hela kwa kumuandika sana kwenye magazeti, kwanza ukiniuliza movie ya mwisho kuiona ya lulu ata sijui ila ukiniuliza lini nimemuona kwenye magazeti ya umbea ntakwambia kila siku...lulu ni msanii wa magazeti sio wa filamu
 
Last edited by a moderator:

Okay........
 
Sio kama namponda ila huo ndo ukweli, kuna maduu wenzie wanakamua haswaa mbele ya camera, Lulu bado sana mkuu

Mkuu hata mbuyu ulianza kama mchicha lulu anazidi kufanya huwezi fananisha na alikotoka. Again hizo pesa anazolipwa ndizo zitamfanya aongeze bidii zaidi katika kuongeza ubora wa kazi zake. Pia usisahau currently anamashabiki wengi which is an important factor in marketing.

Kama ishu ni kuonekana kwenye front pages ya magazeti ya udaku jiulize kwanini yeye. Watu wanaponda magazeti ya udaku but kampuni haijawahi pata hasara. Utakuta mume anayakandia hapa but akifika home ndo kwanza wife yupo bizee anasoma hayo and since marriage is not prison u remain silent.
 

Sijaelewa point yako
 
lulu hajapata producer mzuri tu. pia hajapata stori nzuri ili aonyeshe yeye ni nani. lulu nimeanza kumwona tangu wa hapahapa akiwa na kina yule mama somebody njaidi na wengine. hata katika ffilamu anazocjeza anakuwa real sana na uhusika wake. chunguzeni. tatizo linakuja kwenye bei zake. hatakiwi kutoza hata mil 5. akubali kujishusha ili afanye kazi na watu wanaojua kazi. akingangnia mil 15 atabakia kujitungia stori na kjicast na kujilipa ml 15 na mwisho wa siku atachokwa
 

Kama hujui kausha lulu analipwa milioni 45 kwa movie moja pale proin, usikurupuke kuandikabvitu kama huvijui japo nalukubali mwa u gossip cop wako
 
Kama hujui kausha lulu analipwa milioni 45 kwa movie moja pale proin, usikurupuke kuandikabvitu kama huvijui japo nalukubali mwa u gossip cop wako

Kwi!!! Kwii!!! Kwa kazi gani labda? Au kwa movie IPI? Ebu nijibu hayo maswali mawili kwanza
 
Kama hujui kausha lulu analipwa milioni 45 kwa movie moja pale proin, usikurupuke kuandikabvitu kama huvijui japo nalukubali mwa u gossip cop wako

Unaongea vitu ambavyo huvijui ndugu, pole sana as eh..kama filamu ingekuwa inalipa kiasi hicho usingesikia habar za mabwana wala kugombania wanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…