Lulu‘s “Retrospective 18th Birthday Party’’? katika Picha.

Shadow

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2008
Posts
2,897
Reaction score
675
[h=3]LULU AFANYA BONGE LA PATI[/h]Posted by GLOBAL on April 19, 2013 at 3:35pm 1 Comment 0 Likes
Stori: Imelda Mtema

Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ si mtoto tena, ametimiza rasmi umri wa miaka 18, kilichofuata ni kuangusha bonge la pati ya bethidei, Ijumaa lina mikoba kamili.
Lulu ambaye hivi karibuni aliachiwa kwa dhamana katika kesi ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba aliangusha pati hiyo katika hoteli ya nyota tano ya Serena ya jijini Dar usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, Aprili 17, mwaka huu.…


http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/lulu-afanya-bonge-la-pati
Stori: Imelda Mtema
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ si mtoto tena, ametimiza rasmi umri wa miaka 18, kilichofuata ni kuangusha bonge la pati ya bethidei, Ijumaa lina mikoba kamili.
Lulu ambaye hivi karibuni aliachiwa kwa dhamana katika kesi ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake aliyekuwa mwandani wake, marehemu Steven Kanumba aliangusha pati hiyo katika hoteli ya nyota tano ya Serena ya jijini Dar usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, Aprili 17, mwaka huu.
MAMA LULU NDANI
Shushushu wetu aliyekuwa ndani ya sherehe hiyo alinyetisha kuwa ilihudhuriwa na watu maalum wachache wakiwemo rafiki, wasanii na mama yake mzazi, Lucresia Karugila.
TUMSHUKURU MUNGU
Ilinyetishwa kwamba kabla ya yote, wageni waalikwa waliokuwa na nyuso za furaha walishirikiana na familia ya Lulu kumshukuru Mungu na kumwomba amzidishie staa huyo umri wa kuishi duniani bila vikwazo vya shetani.
“Kikubwa ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa kumfanikisha kufikisha umri wa miaka 18 kwani huko nyuma kulikuwa na maneno mengi juu ya umri wake,” alinyetisha mtu wetu.
NENO LA LULU
Muda mfupi akiwa ukumbini hapo, Lulu alitundika picha za tukio hilo kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika: No more questions (hakuna maswali zaidi)…No more answers (hakuna maji zaidi)…No more lies (hakuna uongo zaidi).
Katika moja ya keki za zoezi hilo kulikuwa na maandishi yaliyosomeka: Happy birthday Lizy “official 18”. Katika sentensi nyingine, maandishi hayo yalimaanisha kuwa amefikisha rasmi miaka 18.
MISOSI, VINYWAJI
Chanzo hicho ambacho
kilifuatilia pati hiyo hatua kwa hatua kilinyetisha kuwa kulikuwa na misosi na vinywaji vya kumwaga ambapo wahudhuriaji walikula na kunywa hadi wakasaza.
LULU MNG’ARO
Kwa macho ya kawaida kabisa, Lulu aling’ara sawia ndani ya gauni refu jeupe lenye kuacha mgongo wazi na kiatu kirefu cha ‘CL’.
“Yaani kiukweli pati ya Lulu ilikuwa bab’kubwa, kwanza ilikuwa ni ya kistaarabu mno na watu wote walipendeza sana akiwemo Lulu mwenyewe. Haikuwa ya kihuni kama wafanyavyo mastaa wengine,” alisema mpashaji wetu.
LULU, KIBA MH!
Katika hali iliyoibua vingi viulizo, Lulu alionekana ‘veri klozi’ na mwanamuziki wa Bongo Fleva aliyewahi kudaiwa kutoka naye, Ali Saleh Kiba ambaye mara nyingi walikuwa wakipiga picha za mapozi wakionyesha furaha waliyokuwa nayo.
Sosi wetu alitonya kuwa hata ulipofika muda wa kukata keki, Lulu na Kiba ndiyo waliiongoza zoezi hilo kisha wakawalisha wageni waalikwa na kugonganisha glasi ‘cheers’.
Lulu yupo uraiani baada ya kukaa nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, Dar kwa takriban miezi 10 akisubiri kesi juu ya kifo cha Kanumba ianze kuunguruma.
 
Hakika sikutegemea angetoka pulic kufanya ushenzi huu. At least angeonesha huzuni kwa marehemu msanii mwenzake. Ajue watu wanamwangalia kwa jicho la ziada. Ushamba ni ushamba tu.
 
Huyu dogo anajaribu kucheza na saikolojia ya mahakimu wa kesi yake waamini kuwa alitenda kosa akiwa na umri wa chini ya miaka 18, maana alishafanya sherehe kama hii miaka miwili iliyopita alimdanganya nani na hili iweje? Kapuuzi haka kabinti kanafurahia ukubwa ili kafanye ufuska wake vizuri maana kamegundua kuwa kaliwahi mno.
 

Tusimlaumu huyu binti kicheche hakika " I have confirmed with 99.99999999% level of confidence" Mama yake hayuko sawa "upstairs" KITUO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…