Lulu: Sipendi "masharobaro"

Lulu: Sipendi "masharobaro"

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee , Elizabeth Michael ' Lulu' amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii , Lulu alisema akiwa na mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.

"Masharobaro hawana nafasi kwangu , kwa sababu hawafikirii maisha kabisa , hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro ," alisema Lulu .
 
Mbona umemind sana, we sharobaro nini.
 
Hahahahaa!awe muwazi tu kwamba masharo hawahongi basi asijifanye maisha sijui nini hapa.
 
Kwelii na hawajui kuhudumia wao wanataka vya bureee,,lakin kuhonga kipajii hhhhhhhhaaaa

Hahahaaa!wasumbufu kama nini masharo!! na kuhonga pia kipaji kama vipaji vingine binamu asikwambie mtu etii... ila nae kazidi jamani hadi mzee mgeni a.k.a ndugu watanzania ptuuu yule si babu yake kabisa. mi sipati picha na lile tumbo eh!mtoto jasiri yule utadhani kanyweshwa ngiloriti.
 
Tena wale mahandsome wakijiangalia kwa kioo muda wote hata pesa hawajui kutafuta,kazi kubadili nguo aonekane yumo kumbe hovyooo
 
Ila wanaume watu wazima kuanzia miaka 35 kuendelea watamu jaman, visharouharo tupa kule lakini Lulu ulizidi komba ni babu kabisaaa

Umeona eeh!mtu kashakula ujana weee akifika 35 na kuendelea akaa hata purukushani zinapungua.
 
Umeona eeh!mtu kashakula ujana weee akifika 35 na kuendelea akaa hata purukushani zinapungua.

Ndio hivyoo wanakua wametulia angalau japo sio wotee, ,
Maana kuna mwingine ana 50 years lakini akili zake ni miaka 18
 
Mtu mzima kashajenga ana watoto wanne wote wanafanya kazi mshahara wake ukiingia unakua hauna kazi zaidi ya starehe, useme nn usipewe.sasa sisi masharo kazi yenyewe kunyoa tumepenga kwa mama amina kodi 30 per month
 
Back
Top Bottom