Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304

Mrembo na mwigizaji wa filamu mwenye mvuto zaidi hapa Bongo (kwa mujibu wa mtandao wa yourbesttop10.com), Elizabeth Michael ‘Lulu' jana usiku aliandika bandiko mtandaoni ambalo liliwaacha midomo wazi baadhi ya mashabiki wake akiwashutumu wanaume wote kuwa wamezaliwa wakiwa tayari wanausaliti na kuwa ni swala la kusubiri ni lini tu atafanya na kuwatahadhalisha wanawake wakaechonjo kwenye mahusiano yao.
Lulu aliandika ujumbe huo kwa lugha ya ‘KIMOMBO' "All men are born hardwired to betray, it's just a question of when! don't get too comfortable".
Kwa wale wafuatiliaji wa tamhilia ya REVENGE ya huko majuu , haya maneno sio mgeni kwao kwani mwanadada Victoria alishawahi kuyatamka. Kutokana na picha ya sura ya upole aliyoibandika kabla ya kuandika maneno haya ilipelekea mashabiki kumuuliza kama amefanyiwa usaliti au.
Huku wengine wakimpa pole, mbali na mashabiki wake kumtaka afunguke zaidi juu ya kile kilichompata mwanadada Lulu hakujibu chochote. Hivi jamani kauli hii ya wanaume wote kujawa na usaliti ndani ni kweli.