MILCAH28
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 1,140
- 327
BAADHI ya wakazi wa kata ya Lumuma, wilaya ya Mpwapwa, wameunga mkono na
kupongeza ushauri waliopewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Kangoye,
kuhusu soko la vitunguu.
Hivi karibuni, mkuu huyo wa wilaya akiwa ziarani katika vijiji vya Lufusi,
Kitati na Mafwene aliwashauri wananchi kuacha kuuza vitunguu mapema, bali
wawe na utamaduni wa kusubiri bei ya soko inapopanda ili iwaongezee kipato.
Kangoye alitoa ushauri huo kutokana na wakulima wengi kukimbilia kuuza
vitunguu mapema kwa bei ya chini, ambapo baada ya muda huanza kuhangaika
kuendesha maisha yao.
MKUU wa wilaya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye
Wakulima hao walisema, tangu walipovuna vitunguu vyao mwezi Agosti, mwaka
jana, waliamua kuvitunza kwenye vichanja vya waziwakisubiri ongezeko la bei
la Januari, Februari na Machi mwaka huu.
Wakati mkuu wa wilaya akituhutubia, tulianza kufikiria itakuwa itakuwa
haina maana kuingiliwa katika mambo yetu binafsi, lakini sasa nadhani
nitafanya mambo makubwa maana bei ya imepanda na kufikia sh. 90,000 kwa
gunia.
Hivi sasa kilimo cha mpunga kinaendelea kufanyika katika bonde la mto Lumuma
Ningeuza wakati ule, ningeambulia sh. 35,000 ambazo zingeishia kwenye
matumizi machache ya nyumbani, alisema Kamilius Ngolelwai, mkazi wa
Mafwene.
Naye Damas Kazi, mkazi wa Lufusi, alisema vitunguu alivyotunza anakusudia
kuviuza wakati wowote kwa bei isiyopungua 100,000 maana ana uhakika siku
chache zijazo vitapanda.
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Lufusi, Jonas Mbogo, alisema watu
walipohamasishwa na mkuu wa wilaya kujifunga mikanda kwa kutouza ovyo
vitunguu vyao, walidhani serikali haikuwa na lengo zuri dhidi yao, lakini
wengi hivi sasa wanapongeza ushauri huo.
Mbogo alisema waliouza mapema vitunguu vyao wamekuwa wakijilaumu baada ya
kuwaona waliovumilia wanaendelea kuvuna fedha nyingi.
Banio mojawapo linalotumika kusafirisha maji kwa wakulima wa mto Lumuma,
wilayani Mpwapwa
Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Lumuma, Joklan Cheliga, alipongeza
ushauri wa DC na kuwataka wapiga kura wake waendelee kuutumia katika misimu
mingine ya kilimo ili wanufaike na jasho lao.
Katika suala hili mkuu wa wilaya amenisaidia hata mimi, maana naweza kukaa
na watu wangu tukapanga mipango ya maendeleo kwa kuwa tuna fedha
zilizotokana na jasho letu, alisema Cheliga.
Akizungumzia suala hilo, Kangoye, alisema ataendelea.. kuwahamasisha wananchi
kutumia rasilimali na fursa walizo nazo kujiletea maaendeleo.
Alisema wakati mwingine umasikini ni wa kujitakia, ikizingatiwa kwamba kata
ya Lumuma ina mto unaotumika kwa kilimo, lakini baadhi ya watu hawautumii
ipasavyo kuwaletea maendeleo.
MAKALA YA NYUMA ILA SI MBAYA TUKIKUMBUSHANA🙂🙂....