Lunch idea: Mchuzi wa kuku wa nazi

Lunch idea: Mchuzi wa kuku wa nazi

brenda18

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
5,687
Reaction score
5,287
Lunch idea... Mchuzi wa kuku wa nazi

Unahitaji:

Kuku wa kienyeji 1
Vitunguu maji 3 (sliced)
Thomu tbs 1 (iliyotwangwa)
1 tsp corriander powder
Nyanya 2 kubwa (chopped)
Curry powder 1 tsp
Nyanya ya kopo (tomato puree) 1 tbs
Tui la nazi zito glass 1
Mtindi kikombe kimoja
Pilipili kavu 1/4 tsp (si lazima)
1 tsp tangawizi mbichi ilosagwa
Chumvi kiasi

Njia:

Chemsha kuku kwa chumvi na thomu mpk aive. Bakiza supu kiasi. Kaanga kitunguu kwa mafuta yalipata moto sana kwa dk 1 tu(visiwe gold).

Vikiiva weka viungo vyote isipokuwa mtindi. Acha mpk viakuke na kukaangika vizuri.

Weka mtindi pamoja na kuku bila supu. Kaanga mpaka wakauke kabisa.

Weka supu uliyobakiza na ikianza kuchemka tu weka tui la nazi.

Acha uchemke mpaka upate uzito uupendao.

Enjoy kwa wali au chapati
 

Attachments

  • 1449742546097.jpg
    1449742546097.jpg
    18.4 KB · Views: 766
Maashallah kwa macho tu huu mchuzi unaonekana mtamu

Thanks brenda18 nami nakuja unibakshie
 
Last edited by a moderator:
Yummmy!! yaonesha mchuzi mzito, mnakula pekee yenu eeeh?!!/ ati hiyo thomu tbs 1 ni nini?!!!

Tutakubakizia swaheeb thomu tbs itakua ni garlic tablespoon (kitunguu saumu kijiko kimoja cha kulia/supu) kama nimekosea brenda18 nisahihishe tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Tutakubakizia swaheeb thomu tbs itakua ni garlic tablespoon (kitunguu saumu kijiko kimoja cha kulia/supu) kama nimekosea brenda18 nisahihishe tafadhali

Ndivyo hivyo hivyo mpenz,karibu..
 
Last edited by a moderator:
brenda18 kumbe unajua kupika mama, okey shukran sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom