Lupaso, Mbezi Beach, Bagamoyo Road

Lupaso, Mbezi Beach, Bagamoyo Road

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Leo nimecheka balaa!

Lakini nimewapongeza makonda daladala wa barabara ya ya Bagamoyo kwa hatua ya kumuenzi baba yetu Mkapa.

Tuko Mezi Goig tonaelekea kituo cha Makonde, konda kaanza:

”Wanaoshuka Lupaso....Lupaso.....Lupaso sogea mbele”

Mie nikapigwa butwaa, mara konda akaongeza:

”Suka ....shusha hapo Lupaso”

Mama mmoja aliyechanganyikiwa akauliza “mie hapo Makonde”
Konda akamdakia:

”Mama tunamuenzi mzee wetu wa ukweli na uwazi, tokea sasa hapa ni Lupaso”

Abiria wote wakacheka mama akitelemka huku naye akicheka.

Makonda wa Dar sina hamu!
 
Inawezekana mzee ana mjengo hapo, ila imakaa vizuri sana
 
Back
Top Bottom