Leo nimecheka balaa!
Lakini nimewapongeza makonda daladala wa barabara ya ya Bagamoyo kwa hatua ya kumuenzi baba yetu Mkapa.
Tuko Mezi Goig tonaelekea kituo cha Makonde, konda kaanza:
”Wanaoshuka Lupaso....Lupaso.....Lupaso sogea mbele”
Mie nikapigwa butwaa, mara konda akaongeza:
”Suka ....shusha hapo Lupaso”
Mama mmoja aliyechanganyikiwa akauliza “mie hapo Makonde”
Konda akamdakia:
”Mama tunamuenzi mzee wetu wa ukweli na uwazi, tokea sasa hapa ni Lupaso”
Abiria wote wakacheka mama akitelemka huku naye akicheka.
Makonda wa Dar sina hamu!