Wabongo mna kazi kweli. Yaani mlichoona kwa mwanamke wa kwanza muafrika kupata tuzo za Oscar ni umbo lake na nguo aliyovaa???? Watanzania punguzeni basi hata huu upumbavu wa kijinga mbaki na ule ambao ni mgumu kuuondoa kwenye akili zenu. Mwenzenu ame-inspire the WHOLE universe nyie mnabaki kumzodoa nguo aliyovaa siku ambayo imebadilisha maisha yake completely. She is now the talk of the world kwa watu maarufu na muhimu duniani na nyie mnabakia kuangalia mambo ambayo kwa watu talented kama hao yanakuwa ya mwisho kuzingatia. Angalieni basi hata twitter yake muone ni watu wa aina gani wamempongeza na hakuna aliyethubutu kuongea ujinga kama mnaoongea nyie maana wako busy kufurahia jinsi binti huyu alivyojitahidi kufika alipofika. Grow up Tanzanians, grow up!!!!!!! "No matter where you are from, your dreams are valid" - Lupita Nyong'o. At least fikirieni basi hata ndoto zenu ni zipi mzifanyie kazi.